Jumapili 12 Aprili 2026 - 15:30
Tunasimama pamoja na watu wetu wavumilivu na mashujaa nchini Lebanon

Hawza/ Hujjat al-Islam wal-Muslimin Sayyid Sadr al-Din al-Qubanchi amelaani uvamizi wa kidhulma uliofanywa na utawala haram wa Kizayuni dhidi ya miji ya Lebanon.

Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Hujjat al-Islam wal-Muslimin Sayyid Sadr al-Din al-Qubanchi, Imamu wa Swala ya Ijumaa wa Najaf Ashraf, kupitia tamko rasmi, amelaani uvamizi uliofanywa na utawala haram wa Kizayuni dhidi ya miji ya Lebanon.

Matini ya tamko hilo ni kama ifuatavyo:

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu

Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na hakika Kwake Yeye tutarejea

Sisi katika janga hili la kibinadamu ambalo watu huru, mashujaa na waumini wa Lebanon wamekumbana nalo kutokana na mashambulizi ya kikatili ya mabomu ya Kizayuni, ambapo mamia ya mashahidi watukufu wamepoteza maisha na maelfu kujeruhiwa, tunashiriki nao katika huzuni na maombolezo yao.

Huku tukilaani uvamizi huu wa dhulma na kukemea ukimya wa kimataifa mbele ya tukio hili, tunasimama pamoja na watu wetu wavumilivu na mashujaa nchini Lebanon.

Tunatoa pole kwa familia za mashahidi watukufu, na tunawaombea majeruhi wapate uponyaji wa haraka.

(وَسَيَعْلَمُ الَّذِينَ ظَلَمُوا أَيَّ مُنقَلَبٍ يَنقَلِبُونَ)

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha