Jumatatu 6 Aprili 2026 - 21:40
Sheikh al-Qattan alaani sera za Utawala harama wa Israrl dhidi ya wafungwa na ametaka hatua ya haraka ya Jumuiya ya kimataifa

Hawza/ Mkuu wa Jumuiya ya “Qawluna wal-‘Amal” na mwanazuoni wa Kisunni wa Lebanon, katika taarifa yake amelaani sera za kihalifu za wavamizi wa Israel dhidi ya kuwanyonga na kuwashikilia wafungwa wa Kipalestina.

Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Sheikh Ahmad al-Qattan, mkuu wa Jumuiya ya “Qawluna wal-‘Amal” na mwanazuoni wa Kisunni wa Lebanon, katika taarifa yake amelaani sera za kihalifu za wavamizi wa Israel ambazo zinafanyika kwa lengo la kuhalalisha kunyongwa wafungwa waliokamatwa wa Kipalestina, na akaitaja hatua hiyo kuwa ni “unyama na kuporomoka kwa maadili” kunakokanyaga maadili yote na mikataba ya kimataifa.

Alisisitiza kuwa; ugaidi huu uliopangwa dhidi ya wafungwa ni sura nyingine ya uadui na mashambulizi ya mara kwa mara ya adui Mwisraeli dhidi ya nchi yetu ya Lebanon, na unaonesha fikra za kihalifu zisizothamini maisha ya binadamu wala kuheshimu mamlaka ya nchi.

Sheikh al-Qattan aliiita Jumuiya ya kimataifa, mashirika ya haki za binadamu na nchi zote za Kiarabu na Kiislamu kuunganisha safu zao na kubeba majukumu yao ya kimaadili na kisheria kwa kuchukua hatua za haraka ili kusitisha maamuzi haya ya kidhalimu na kuzuia uchokozi wa Israel.

Mwanazuoni huyo wa Kisunni wa Lebanon pia alitaka juhudi za dhati zifanywe ili kuwafikisha mahakamani wahusika wa uhalifu huu katika mahakama za kimataifa kwa lengo la kuokoa maisha ya wasio na hatia, na akasisitiza kuwa; ukimya mbele ya yale wanayokabiliana nayo wafungwa na Lebanon ni mtihani halisi kwa dhamiri iliyosalia ya Jumuiya ya kimataifa.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha