Jumapili 29 Machi 2026 - 15:54
Ayatullah A'rafi amewataka wanazuoni katika ulimwengu wa Kiislamu kuonesha mshikamano dhahiri, wa wanazuoni wa Kiislamu na dini mbalimbali katika kipindi hiki cha kihistoria

Hawza/ Hujjatul-Islam wal-Muslimin Husayni Kuhsari, huku akirejea barua za shukrani na pongezi kutoka kwa Mkurugenzi wa hawza Iran, kwa ajili ya uungaji mkono na msimamo wa wanazuoni wenye ushawishi na athari katika fikra za umma wa ulimwengu wa Kiislamu, alisema: Ayatollah A'rafi amewataka wanazuoni katika ulimwengu wa Kiislamu kuonesha mshikamano dhahiri wa wanazuoni wa Kiislamu na wa dini mbalimbali katika kipindi hiki cha kihistoria.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Mufid Husayni Kuhsari katika mahojiano na Shirika la Habari la Hawza, huku akifafanua barua za shukrani na pongezi za Ayatollah A'rafi, Mkurugenzi wa hawza, kwa ajili ya uungaji mkono na misimamo ya wanazuoni wenye ushawishi na athari katika fikra za umma wa ulimwengu wa Kiislamu kuhusu shambulio la kivamizi la Marekani  na utawala wa Kizayuni dhidi ya nchi ya Iran, na kumuua shahidi kiongozi wa taifa na watu wasio na hatia, alisema: Ayatullah A'rafi katika ujumbe wake amewataka wanazuoni wa ulimwengu wa Kiislamu kuonesha mshikamano wa wazi wa wanazuoni wa Kiislamu na wa dini mbalimbali  zaidi katika kipindi hiki cha kihistoria.  

Ameendelea kusema kuwa: Ayatullah A'rafi katika barua zake alieleza kuwa; ukubwa na kina cha jinai hii havijifichi kwa wenye basira, na kumlenga kwa makusudi marji' wa taqlid na kimbilio la Mashia, kiongozi wa kidini na cheo cha juu kabisa cha kisiasa cha Jamhuri ya Kiislamu, pamoja na mauaji ya watoto na raia wasio na ulinzi na mashambulizi dhidi ya miundombinu muhimu, ni janga lisilo na mfano ambalo limekengeuka kabisa kanuni na misingi yote ya kimataifa.  

Naibu wa masuala ya kimataifa wa hawza ameongeza kusema: Mkurugenzi wa Vyuo vya Dini, kwa kubainisha kuwa; sisi ndani ya hawza na watu wa Iran tumehuzunishwa na kuuwawa kiongozi wetu mpendwa na watoto wasio na hatia wa ardhi hii, aliwaandikia viongozi wa kimataifa kwamba; katika msiba huu mkubwa, macho ya watu wa Iran na Waislamu ulimwenguni, yameelekezwa kwa wanazuoni wa dini katika pande zote za dunia, ili kwa misimamo yao yenye hekima, watimize jukumu lao la kihistoria katika kuitetea nafsi na hadhi ya wanazuoni na usafi wa watoto wa umma wa Kiislamu.  

Hujjatul-Islam wal-Muslimin Husayni Kuhsari alisema: Katika barua hizi, sambamba na kutoa shukrani na pongezi kwa uungaji mkono na misimamo ya wanazuoni wenye ushawishi na athari katika fikra za umma wa ulimwengu wa Kiislamu, imetakiwa kwamba muifikishe sauti ya dhulma hii zaidi ya mipaka ya kimadhehebu, kidini na kijiografia mpaka ulimwengu usikie.  

Akaongeza kusema: Ayatullah A'rafi katika diplomasia ya mawasiliano alifafanua kwamba; katika jinai hii shambulio dhidi ya heshima ya Marjaiyyah na uongozi wa kidini kwa ujumla wake ni tishio ambalo hakuna dini itakayokuwa salama dhidi ya athari zake, na alionesha matumaini kwamba; kwa kukemea wazi na kwa uthabiti jinai hizi, mshikamano wa wanazuoni wa Kiislamu na wa dini mbalimbali katika kipindi hiki cha kihistoria utaonekana zaidi.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha