Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Kata’ib Sayyid al-Shuhada imetuma ujumbe wa rambirambi kwa familia ya Dkt. Ali Larijani, kwa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, na kwa watu wa Iran kwa ujumla, ikisema:
Bismillah al-Qasim al-Jabariin
“Na yeyote atakayepigana katika njia ya Mungu, akauawa au kushinda, tutamjalia malipo makubwa.
” (Qur'ani, Surah An-Nisa, 74)
Harakati ya Kiislamu ya Kata’ib Sayyid al-Shuhada inatoa pole kutokana na shahada ya mwanazuoni na mchapakazi Dkt. Ali Larijani, Katibu Mkuu wa Baraza la Juu la Usalama wa Taifa la Iran, kwa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi, kwa watu shujaa wa Iran, na kwa familia yake.
Shahidi Ali Larijani alikuwa mfano bora wa malezi kutoka katika shule ya muqawama ya Kiislamu, na miaka yake mingi ya uwepo wake mstari wa mbele katika kulinda Uislamu na Mapinduzi ilikuwa ni mwiba kwa maadui. Ujasiri wake pamoja na upevu wake wa akili na maono katika medani za upinzani ni mfano unaoendeshwa na wapiganaji wa Kiislamu.
Maadui wa Kizayuni na Marekani, ambao wamefikia kikomo katika vita visivyo vya haki dhidi ya umma wa Kiislamu, wanadhani kuwa kwa kumuua Dkt. Larijani na wenzake, watadhoofisha mapambano ya muqawama. Lakini hawajui kuwa shahada ni moja ya maombi ya wapiganaji wa muqawama ambao kila wakati wanaiomba kwa Mungu wao.
Licha ya kwamba habari ya shahada ya Dkt. Larijani ni ya kuhuzunisha na kutia uchungu mkubwa kwenye jamii ya Kiislamu, njia ya muqawama, na watu wa Iran, maadui wanapaswa kujua kuwa; mauaji haya ya kikatili hayatadhoofisha dhamira thabiti ya umma wa Kiislamu katika kuiangamiza kambi ya kikafiri, bali yataimarisha dhamira yetu ya kurejesha kisasi kikali na chenye maumivu.
“Na tulilipiza kisasi kwa wale waliotenda uovu, na ilikuwa haki juu yetu kuwasaidia waumini.
” (Qur'ani, Surah Ar-Rum, 47)
Harakati ya Kiislamu ya Kata’ib Sayyid al-Shuhada, Iraq
Maoni yako