Jumamosi 14 Machi 2026 - 00:30
Kiongozi wa Ansarullah Yemen ampongeza Ayatullah Sayyid Mujtaba Khamenei kwa kuchaguliwa Kiongozi wa Mapinduzi ya Iran

Hawza/ Sayyid Abdul-Malik al-Houthi, kiongozi wa Ansarullah Yemen, ametoa pongezi kwa kuchaguliwa kwa Ayatullah Sayyid Mujtaba Khamenei kuwa kiongozi wa tatu wa Mapinduzi ya Iran.

Kwa mujibu wa kitengo cha kimataifa cha Shirika la Habari la “Hawza”, Sayyid Abdul-Malik al-Houthi, kiongozi wa harakati ya Ansarullah ya Yemen, ametoa pongezi kwa taifa la Iran, taasisi rasmi za nchi hiyo pamoja na vikosi vyake vya ulinzi kwa kuchaguliwa Ayatullah Sayyid Mujtaba Khamenei kuwa kiongozi wa tatu wa Mapinduzi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Alieleza kuwa; kuafikiwa kwa tukio hili ni pigo kubwa kwa matwaghuti wa zama hizi, yaani Marekani na Israel, na pia ni sababu ya kukata tamaa kubwa kwao.

Kiongozi wa Ansarullah pia alisisitiza msimamo thabiti na mshikamano wa harakati hiyo pamoja na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na watu Waislamu wa Iran katika kukabiliana na uchokozi na ubeberu wa Marekani na Israel.

Chanzo: Tasnim.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha