Hujjatul-Islaam Ahmad Farkh Fa'l, katika mazungumzo yake na Shirika la Habari la Hawza, huku akitoa pole kutokana na Shahada ya Kiongozi Mtukufu Ayatullah Imam Khamenei (ra) amesema: Kiongozi Mtukufu wa Mapinduzi, mara nyingi alikuwa akimuomba Mola amruzuku Shahada na leo hii Mwenyezi Mungu Mtukufu Shahada hii tukufu amemzawadiwa Kiongozi huyu adhimu.
Huku akisisitiza kuwa Taifa la Iran limejengeka kwa kufuata misingi ya sheria iliyoundwa na Wilayat Faqih, alisema: Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, unataka kusimika Uislamu asilia, na Taifa lenye nguvu la Iran vile vile ni Taifa kubwa likiambatana na Mfumo wa Kiislamu.
Kiongozi wa shura ya juu ya Hawza aliendelea kusema: Kinacho takiwa kukizingatia ni hichi kwamba, sisi sote malengo ya nidhamu ya Kiislamu tusiyaache na kwa kupigana jihadi tusalie kwenye njia hii.
Hujjatul-Islaam Farkh Fa'l, alidhihirisha kuwa: Wakati Imam Khomein alipoileta fikra ya Wilayatul-faqih na Uislamu asili, uhalisia wa uovu wa Marekani na Mashia wa London ulidhihiri. Muamko wa Uislamu ambao leo hii tunaushuhudia ni tija ya nuru ya Mapinduzi ya Kiislamu, hivyo basi; watu ambao watapata shahada katika kutimiliza malengo makubwa ya Mapinduzi haya ambayo ni kuhuisha Uislamu asili, basi watakuwa na daraja ya tofauti kabisa.
Hujjatul-Islaam Farkh Fa'l amesema: Muda wa kuwa Viongozi wa mrengo wa haki vitu vyao vyote wanavitoa kwa ajili ya Uislamu na Qur'ani, Uislamu hauwezi kusimama. Muda wa kuwa shakhsia mfano wa Imaam Khamenei katika njia hii wanapata Shahada, haitawezekana kusita katika njia hii.
Yeye amedhihirisha kuwa: Malezi yaliyopatikana kutoka kwa Mtukufu Imam Khamenei, leo hii ndani ya Irani na kwenye nchi nyengine yanahifadhi maslahi ya Uislamu, hivyo basi, njia ya Shahada mpaka atakapo dhihiri Imam wa Zama (as) haiwezi kusitishwa na Shahada hizi ndizo zinazo uhifadhi Uislamu.
Akisisitiza kuwa leo hii makabiliano kati ya mrengo wa haki na batili yamefikia hatua kwamba mirengo hii miwili inatunishiana misuli, aliashiria: Jamhuri ya Kiislamu ya Irani, siku hizi inapigana na nchi zenye kujimwambafai ulimwenguni, na shahada ya Imaam Khamenei imekuwa chachu ya kutia nguvu na ushindi kwenye mrengo wa haki dhidi ya mrengo wa batili, na dunia ya wenye kutakabari itashuhudia tija ya ushindi wa vita hii, tija ambayo itakuwa ni kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Irani.
Kiongozi wa shura ya juu ya Hawza alidhihirisha kuwa: Jamhuri ya Kiislamu baada ya kushinda katika vita hivi vya kulazimishwa itabadilika kuwa ni mwenye nguvu ulimwenguni na mambo yote na siasa katika ukanda huu zitapangwa kwa mtazamo wa Iran.
Kwa maelezo ya Hujjatul-Islaam Farkh Fa'l, Iran baada ya kushinda katika vita hivi vya kulazimishwa haitakuwa tena Irani hii tuliyonayo leo, bali itabadilika kuwa mchezaji mwenye nguvu na mwenye athari ulimwenguni, kwa sababu imesimama dhidi ya mabeberu wa ulimwengu na kuwashinda.
Mjumbe wa Jumuiya ya Hawza ya Qum, pia amezihutubia nchi jirani kwa kusema: Nchi jirani ni lazima zipige mahesabu ya baada ya vita na zifahamu kwamba, Amerika hatokuwa na nafasi yeyote kwenye mstakabali wa ukanda huu, na si wa kutegemewa na pia hatokuwa na uwezo wa kuzikingia kifua nchi hizo. Hivyo basi; nchi hizo inabidi zitekeleze wadhifa wao na ziungane ili kukabiliana na adui wa Uislamu.
Maoni yako