Jumapili 1 Machi 2026 - 21:26
Muqtada Sadri, atuma salamu za rambirambi kutokana na Kupata Shahada Kiongozi wa Mapinduzi ya Iran/ Atangaza siku tatu za maombolezo Iraqi

Hawza/ Kiongozi wa Harakati ya Sadri nchini Iraqi, kwa kutoa ujumbe kutokana na kupata Shahada Kiongozi wa Mapinduzi, ametuma salamu za rambirambi kwa Waislamu wote.

Kwa mujibubwa Shirika la Habari la Hawza,Muqtada Sadri, Kiongozi wa Harakati ya Sadri nchini Iraqi, kwa kutoa ujumbe kutokana na kupata Shahada Kiongozi wa Mapinduzi, ametuma salamu za rambirambi na kusema:

Kwa huzuni na masikitiko makubwa, natoa salamu zangu za rambirambi kuulelekea ulimwengu wote wa Kiislamu, kutokana na kupata Shahada Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, Mwanazuoni Mchamungu na mwenye kujizatiti katika Jihadi.

Kwa kuitengemea aya ya Mwenyezi Mungu isemayo:


من المؤمنین رجال صدقوا ما عاهدوا الله علیه…»


Amewapa pole waislamu wote kutokana na msiba huu, na amemuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu, amueke katika daraja ya Mashahidi na wenye kusema ukweli, na amfufue pamoja na watoharifu.

Muqtada Sadri kutokana na msiba huu, ametangaza rasmi siku tatu za maombolezo nchini Iraq.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha