Ijumaa 20 Februari 2026 - 07:00
Qatar yazindua kituo cha televisheni cha usomaji wa Qur’ani

Hawza/ Kampuni moja ya vyombo vya habari ya Qatar imetangaza uzinduzi wa Kituo cha Qur’ani cha Qatar katika siku ya kwanza ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani mwaka huu.

Kwa mujibu wa Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, kituo hiki kipya cha televisheni kitajikita katika kurusha usomaji wa Qur’ani Tukufu kwa muda wa masaa ishirini na nne.

Sheikh Khalid bin Abdulaziz bin Jassim Al Thani, Mkurugenzi Mtendaji wa Qatar Media Corporation, alieleza kuwa; hatua hii ni mkakati wa ndani ya mfumo wa mpango uliopangwa wa kupanua vituo maalumu vyenye maudhui lengwa.

Alisema: Kituo hiki kinaakisi dhamira ya kampuni hii ya vyombo vya habari katika kuwasilisha maudhui ya Qur’ani yenye ubora wa hali ya juu na kusaidia kueneza utamaduni wa Qur’ani kupitia majukwaa ya vyombo vya habari vilivyopo.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji huyo, timu za maandalizi zimefanya juhudi kubwa kuhakikisha utayari wa kiutendaji wa mradi huu, ikiwa ni pamoja na uteuzi makini wa visomo vya Qur’ani, ambavyo vimepitishwa katika uchunguzi wa kitaalamu ili kuhakikisha ubora na usahihi wake.

Chanzo: The Peninsula

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha