Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Asif Ali Zardari, Rais wa Pakistan, katika hafla iliyofanyika kutokana na mnasaba wa maadhimisho ya miaka arobaini na saba ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran mjini Islamabad, mji mkuu wa Pakistan, alisisitiza kina cha uhusiano kati ya nchi hizo mbili na kusema: Mahusiano kati ya Iran na Pakistan yana mizizi katika historia, lugha, utamaduni na jiografia ya pamoja, na katika miaka iliyopita yameendelea kuimarishwa na kutiwa nguvu zaidi.
Vilevile, alieleza matumaini kwamba roho ya udugu na ushirikiano kati ya nchi hizo mbili itaendelea kupanuka katika miaka ijayo, na itachukua nafasi yenye athari chanya katika kufanikisha ustawi, uthabiti na mshikamano kwa manufaa ya mataifa yote mawili na eneo zima kwa ujumla.
Maoni yako