Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Sadruddin Qabanchi, Imamu wa Swala ya Ijumaa ya Najaf Ashraf, katika hotuba za Swala ya Ijumaa alizozitoa kwenye Husseiniyya Kuu ya Fatimiyya mjini Najaf Ashraf, alisisitiza: Mafanikio ya mchakato wa kisiasa nchini Iraq, yaliyopatikana kwa kuchaguliwa Spika wa Bunge la Wawakilishi na manaibu wake wawili, na sasa tukisubiri kuchaguliwa Rais wa Jamhuri kisha Waziri Mkuu, yanaonyesha kuwa mambo yanaendelea kwa ushirikishwaji mpana, mafanikio endelevu na kwa mifumo sahihi.
Imamu wa Ijumaa wa Najaf Ashraf, katika maneno yake kutokana na mnasaba wa kumbukumbu ya kuuawa kishahidi makamanda wa ushindi, alisema: Kwa nini tunawakumbuka mashahidi hawa wawili watukufu? Kwanza, ili kusisitiza usahihi wa njia; na pili, ili kuthibitisha kuendelea kwa njia hii.
Akiashiria kwamba mashahidi hawa wawili ni mfano halisi wa Aya Tukufu: «رِجَالٌ صَدَقُوا مَا عَاهَدُوا اللَّهَ عَلَیْهِ» alisema: Leo tunaishi katika neema ya usalama kwa baraka ya damu za mashahidi; hakuna kurudi nyuma katika njia hii, wala hakuna hofu kuhusu mustakabali; kwani “Na Mwenyezi Mungu ndiye Mshindi juu ya jambo Lake” (وَاللهُ غَالِبٌ عَلَی أَمرِهِ), na hivi karibuni Iraq itacheza jukumu muhimu katika kubadilisha ramani ya dunia.
Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Sadruddin Qabanchi, katika sehemu nyingine ya hotuba, akijibu swali: Ni vipi Iraq inapaswa kutazamwa katika mwaka wa 2026 Miladia? Alisema: Tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu mwaka huu uwe kituo cha kuundwa kwa serikali, utoaji wa huduma, ujenzi na maendeleo ya kiuchumi.
Aliongeza: Sambamba na maadhimisho ya kuzaliwa kwa Amirul-Mu’minin Imam Ali (a.s.), tunatarajia mwaka huu uwe kituo cha ukuaji na maendeleo zaidi katika njia ya kidini ya taifa letu, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Khatibu wa Ijumaa wa Najaf Ashraf, katika hotuba ya kidini kutokana na mnasaba wa maadhimisho ya kuzaliwa Imam Amirul-Mu’minin Ali (a.s.) ndani ya Kaaba, alisema: Tukio hili si la kihistoria na la kupita tu, bali ni tukio la juu ya ubinadamu na la kiungu.
Akielezea sababu ya kuwa na ufuasi (wilaya) kwa Imam Amirul-Mu’minin Ali (a.s.), alisema: Kwa kutegemea Hadithi Tukufu ya Mtume Mtukufu (s.a.w.) aliyesema:
“Ewe Ali, hakuna anayekupenda isipokuwa Muumini, na hakuna anayekuchukia isipokuwa mnafiki,”
basi ufuasi wa Amirul-Mu’minin (a.s.) kwa hakika ni ufuasi wa Mwenyezi Mungu.
Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Sadruddin Qabanchi pia, katika sehemu nyingine ya hotuba yake akizungumzia Mwaka Mpya wa Miladia, alisema: Katika Sheria ya Kiislamu kuna sikukuu rasmi tatu tu: Iddi ya Adh-ha, Iddi ya Fitri na Iddi ya Ghadir Khum; na katika sikukuu hizi, waja hujitahidi kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu.
Alisisitiza kuwa: Katika Uislamu hakuna sikukuu ya kisheria inayohusiana na kuanza mwaka wa Miladia.
Maoni yako