Ijumaa 2 Januari 2026 - 00:00
Kuwaheshimu wanazuoni na wasomi ni wajibu wa kimaadili

Hawza/ Ayatullah Al-‘Udhma Ja‘far Subhani, katika ujumbe wake kwenye hafla ya kumuenzi Profesa Muhammad Ali Mahdavi-Rad, ameeleza kuwa; kuwaheshimu wanazuoni na wasomi ni wajibu wa kimaadili.

Kwa mujibu wa  Shirika la Habari la Hawza, maandishi kamili ya ujumbe huu uliotolewa katika hafla ya kumuenzi Profesa Muhammad Ali Mahdavi-Rad, iliyofanyika Alhamisi tarehe 1 January 2026 katika Ukumbi wa Utamaduni wa Chuo cha Farabi, ni kama ifuatavyo:

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu

Wanazuoni na wasomi, ambao ni taa na nuru ya elimu na utamaduni, wanafanana na watu waliobeba taa mikononi mwao wanaowaangazia njia wale wanaotembea katika safari ya utafiti, na jamii hunufaika kutokana na fikra na tafiti zao.

Kwa hiyo, kuwaheshimu ni wajibu wa kimaadili; kama vile kumheshimu mwalimu kwa watu wote waliyonufaika na elimu yake kunavyochukuliwa kuwa ni jukumu la dhamiri.

Katika riwaya kutoka kwa Imam Hasan Askari (amani iwe juu yake) imeelezwa kuwa, alipomjia mwanazuoni kwenye baraza, alimpa nafasi ya juu kuliko jamaa zake wote na akamkalisha mbele ya baraza. Alipoulizwa na kukosolewa kuhusu mwenendo huo, Imam alijibu: “Yeye” kwa utetezi wa kielimu na hoja thabiti huwafedhehesha na kuwashinda maadui.

Mwanazuoni mahiri Hujjatul-Islam wal-Muslimin Mahdavi-Rad ni miongoni mwa mifano iliyo wazi ya kanuni hii. Tangu ujana wake hadi leo, ameendelea kufanya tafiti zenye thamani katika nyanja mbalimbali za utamaduni wa Kiislamu; hususan kazi zake za Qur’ani na historia ambazo ni za mwangaza mkubwa na zenye kuonesha njia.

Aidha, katika mbinu za utafiti pia ni mbunifu. Jarida la Ayin-e Pazhuhesh ni miongoni mwa ubunifu wake, ambalo kwa bahati nzuri limeendelea kuchapishwa kwa mtiririko hadi leo.

Mimi, nawapelekea salamu na pongezi wote waliokuwa na mchango katika kuienzi shakhsia hii ya kielimu ya hawza na chuo kikuu, na namuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu amjaalie Mtukufu Mahdavi-Rad mafanikio yanayoongezeka kila siku. Natumaini atapokea pongezi hizi chache kutoka kwangu, kwani kwa hakika hadhi yake ya kielimu inastahili zaidi ya hayo.

Ja‘far Subhani

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha