Alhamisi 1 Januari 2026 - 20:00
Pakistan yakataa vikali hatua ya utawala wa Kizayuni kuhusu Somaliland

Hawza/ Tahir Hussein Andarabi, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Pakistan, katika taarifa rasmi, huku akilaani vikali juhudi zozote za kudhoofisha mamlaka na umoja wa ardhi ya Somalia, alitangaza kuwa; Islamabad inachukulia tamko la utawala wa Kizayuni kuhusu kuitambua Somaliland kuwa ni hatua isiyo halali, ya kichochezi na inayopingana na sheria za kimataifa.

Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Tahir Hussein Andarabi, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Pakistan, alisema katika taarifa yake: Pakistan inalaani vikali jaribio lolote la kuchafua au kudhoofisha mamlaka, umoja na ukamilifu wa ardhi ya Somalia, na inakataa kwa uthabiti tamko la utawala wa Kizayuni la kulitambua eneo la “Somaliland” kama nchi huru.

Ameeleza kuwa; hatua hiyo ya utawala wa Kizayuni ni kinyume cha sheria, ni ya kichochezi na inapingana na misingi na kanuni zilizokubalika za sheria za kimataifa, akisisitiza kuwa hatua kama hizo si tu tishio kubwa kwa amani na uthabiti wa nchi rafiki na ndugu ya Somalia, bali pia zinaweka hatari usalama na utulivu wa eneo zima.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Pakistan, akirejelea wajibu wa jumuiya ya kimataifa, ameitaka ichukue msimamo thabiti wa kukataa hatua za aina hii, na akasisitiza: Jumuiya ya kimataifa inapaswa kuzuia utawala wa Kizayuni kudhoofisha, kupitia vitendo vyake, juhudi zinazoendelea za kulinda na kuimarisha amani na uthabiti katika eneo hilo.

Mwisho wa taarifa hiyo unasema: Pakistan inatangaza uungaji mkono wake kamili kwa mamlaka, umoja na ukamilifu wa ardhi ya Somalia, pamoja na kuunga mkono juhudi zote za kufanikisha amani na uthabiti wa kudumu katika nchi hiyo.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha