Alhamisi 1 Januari 2026 - 18:44
Korea Kusini yaandaa chakula cha halali kwa ajili ya watalii waislamu

Hawza/ Mgahawa unaoandaa vyakula vya halali kwa Waislamu ulipokelewa kwa shauku kubwa na wanafunzi wanaoishi Korea Kusini, na baadaye ukapata umaarufu pia miongoni mwa watalii Waislamu. Kwa sasa, mgahawa huo unamiliki takribani asilimia 70 ya mchango katika kuwavutia Waislamu wanaofika Korea.

Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, kutokana na kuongezeka kwa matangazo ya Korea katika kueneza utamaduni wa nchi hiyo kupitia sekta ya utalii, Waislamu wengi zaidi kutoka sehemu mbalimbali duniani wanafika Korea kwa ajili ya kutembea, jambo ambalo limesababisha kuongezeka kwa migahawa na vituo vya kuandaa vyakula vya halali kwa ajili ya Waislamu.

Hata hivyo, ni migahawa 15 tu rasmi ya kuandaa chakula cha halali ambayo imepata vyeti vya uthibitisho kutoka Kituo cha Kiislamu cha Korea. Migahawa ya mtandao ya “Halal Pasand” hutambulishwa baina yao kupitia mitandao ya kijamii miongoni mwa wananchi na watalii, na migahawa hii imepata uwepo na nafasi hai ndani ya jamii ya Waislamu wa Korea.

Chanzo: THE CHOSUN

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha