Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, maandishi kamili ya ujumbe wa Ayatullah Alireza A‘rafi uliotolewa kwenye hafla ya kumuenzi Profesa Muhammad Ali Mahdavi-Rad, iliyofanyika Alhamisi tarehe 1 January 2026 katika Ukumbi wa Utamaduni wa Chuo cha Farabi, ni kama ifuatavyo:
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu
Kuenzi shakhsia adhimu ya Profesa Hujjatul-Islam wal-Muslimin Mahdavi-Rad ni hatua yenye baraka kubwa. Sisi, kama Hawza ya Kielimu, tunawashukuru na kuwathamini kwa dhati wapendwa wote waliochukua juhudi za kuandaa hafla ya heshima na pongezi kwa msomi huyu mpendwa na mwenye hekima.
Ninayo heshima ya kuwa nimekuwa na uhusiano na mawasiliano naye tangu zamani, kwa karibu na kwa mbali, na nimefaidika na hoja na mijadala yake, kwa njia ya moja kwa moja na isiyo ya moja kwa moja.
Dkt. Mahdavi-Rad ana sifa ya kuelewa kwa kina maktaba ya Mashhad na maktaba ya Qum kwa pamoja. Katika kipindi alichokuwa akisoma katika Hawza ya Kielimu ya Mashhad, hawza hiyo, kwa uwepo wa marehemu Ayatullah al-‘Udhma Milani na shakhsia nyengine nyingi hai za kielimu, ilikuwa na nafasi nzuri na yenye harakati katika mijadala ya kielimu. Sambamba na hilo, hawza hiyo ilikuwa na msukumo mkubwa katika nyanja za kitamaduni na kijamii, kiasi kwamba uwepo wa shakhsia kubwa kama Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika hawza hiyo uliongeza ari, hamasa na uhai wa kielimu, kitamaduni na kijamii.
Zaidi ya kuwa Hawza ya Mashhad ilikuwa na historia ndefu na utajiri mkubwa katika fasihi ya Kiarabu, Profesa Mahdavi-Rad alizielewa sifa na fadhila hizi za hawza ya Mashhad na alikuwa na ufahamu wa karibu wa mitazamo na mielekeo yake mbalimbali.
Ukaribu na uhusiano wake na Qur’ani Tukufu, sambamba na nyanja nyingine zilizotajwa, uliunda mizizi yake huko Mashhad. Baadaye, kwa kuhamia Qum, alifahamiana na mielekeo mbalimbali ya kielimu ya Qum katika itikadi, falsafa, fiqhi, hadithi na tafsiri, na akapata uelewa mzuri na wa kina katika viwango vya juu katika nyanja tofauti za elimu za Kiislamu huko Qum.
Kuelewa misingi miwili na shule mbili za kielimu kutoka hawza mbili, hususan hawza ya Mashhad ya kipindi hicho, ni miongoni mwa alama muhimu katika historia yake ya kielimu na katika shakhsia yake ya kielimu na kifikra.
Profesa Mahdavi-Rad ni mwanazuoni wa kijamii, aliyehusika moja kwa moja na masuala ya kifikra, kitamaduni, kijamii na kisiasa ya nchi katika miongo kadhaa — kuanzia zama za harakati za Imam Khomeini (rehma ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake), hadi Mapinduzi ya Kiislamu, na baada ya hapo kuundwa kwa Mfumo wa Kiislamu na kuibuka Mapinduzi ya Kiislamu.
Pamoja na kuwa ni mwanafunzi mwenye bidii na aliyeelimika katika fiqhi, usul, fasihi na masuala mbalimbali ya hawza, kwa uelewa na busara alielekeza mkazo wake katika mhimili na kitovu cha Qur’ani na Hadithi.
Kwa hakika, licha ya hali yake nzuri ya kielimu katika nyanja mbalimbali za elimu za Kiislamu na hawza, msisitizo wake juu ya Qur’ani na Sunna ni nukta angavu katika mapokeo ya kielimu, maisha na mwenendo wake wa kielimu.
Yeye, pamoja na kuwa mtafiti na mchunguzi mwenye thamani na anayeaminika, ana uwezo mzuri wa kusimamia utafiti, kuongoza miundombinu ya utafiti na kusukuma mbele miradi mikubwa ya utafiti.
Wakati huohuo, hakuingia katika nyadhifa za kiutendaji wala hakutaka kuingia humo; lakini katika usimamizi wa matukio na mchakato wa kielimu kama vile Tuzo ya Kitabu cha Mwaka na mengineyo, aliingia kwa njia ya kielimu, yenye nidhamu na yenye manufaa.
Vivyo hivyo, katika uongozi wa miradi mikubwa ya utafiti na tafiti za kina, pamoja na kusimamia kazi za pamoja na za vikundi katika utafiti, ana uwezo na ujuzi wa thamani kubwa.
Pamoja na fadhila zake za kielimu, mtazamo wake mpana, mielekeo ya kimataifa, uongozi wake wa utafiti na athari chanya alizoziacha katika anga ya mijadala mbalimbali ya kielimu kwenye hawza na vyuo vikuu — ambapo wanafunzi wengi wa vyuo na wa hawza wamenufaika naye, pamoja na kalamu, hotuba na miongozo yake, na vitabu na kazi nyingi nzuri zimeandikwa — lakini kinachovipa vyote hivi mwanga na uzuri wa pekee ni maadili yake mema, tabia yake ya juu, mwenendo wake wa kijamii na kiroho.
Miongoni mwa misingi mikuu ya kuwa mwanahawza ni kuwa na mtazamo wa mbinguni, mwelekeo wa kiirfani na kushikamana na thamani za kimaadili, na kudhihirisha hayo katika mwenendo wa mtu katika uhusiano wake na Mwenyezi Mungu, na watu, na katika mahusiano yake na watafiti na wanafunzi wa elimu. Sifa hizi nyingi za kimaadili na fadhila mbalimbali zinaonekana wazi katika mtindo, mwenendo na matendo yake, na hilo linastahili pongezi na heshima.
Kwa mara nyingine tena, tunamshukuru na kuithamini shakhsia hii mkubwa, na tunamuombea afanikiwe. Insha’Allah aendelee kudumu, na baraka ya elimu yake, juhudi zake za kielimu na uongozi wake wa kielimu viendelee. Mwishoni, kwa mara nyingine tena nawapongeza na kuwashukuru waandaaji wote wa hafla hii ya heshima, wahudhuriaji, waandishi wa makala na wahadhiri.
Maoni yako