Shirika la Habari la Hawza — Amirul-Mu’minin (as) katika kauli yake yenye nuru ameashiria matokeo mabaya ya tabia mbovu ya kimaadili inayoitwa tamaa, akasema:
«أَزْرَى بِنَفْسِهِ مَنِ اسْتَشْعَرَ الطَّمَعَ»
“Yeyote anayefanya tamaa kuwa desturi yake, amejidhalilisha mwenyewe.” (3)
Sherehe:
 Neno “tamaa” linamaanisha kutaka zaidi ya haki yako na kujaribu kupata neema za maisha kupitia wengine. Neno “istash‘ara” linamaanisha “kuvaa nguo ya ndani”, likionesha kwamba mtu mwenye tamaa ameambatana nayo kwa karibu kiasi cha kutoweza kujitenga nayo. Ni jambo lililo wazi kwamba watu wenye tamaa, kwa ajili ya kutimiza malengo yao, watalazimika kukubali udhalili, kuombaomba kwa kila mtu, na kuvunja utu na heshima yao.
Ahadi ya furaha katika Qur’ani:
Mwenyezi Mungu katika Qur’ani Tukufu amewaahidi waja wake waumini ahadi ya furaha ya macho. zawadi ambayo hakuna mtu anayeijua isipokuwa Yeye tu. Anasema:
«فَلَا تَعْلَمُ نَفْسٌ مَا أُخْفِیَ لَهُمْ مِنْ قُرَّةِ أَعْیُنٍ جَزَاءً بِمَا کَانُوا یَعْمَلُونَ.»
“Hakuna nafsi inayojua malipo makubwa yaliyofichwa kwayo — ambayo yatakuwa ni furaha ya macho — kwa yale waliyokuwa wakiyafanya.” (4)
Ili kuipata furaha hii, moja ya maelekezo ni kujiepusha na tamaa. Kama alivyosema Imam As-Sadiq (as):
«إِنْ أَرَدْتَ أَنْ تَقَرَّ عَیْنُکَ وَ تَنَالَ خَیْرَ الدُّنْیَا وَ الْآخِرَةِ فَاقْطَعِ الطَّمَعَ عَمَّا فِی أَیْدِی النَّاسِ.»
“Kama unataka macho yako yawe na furaha, na upate kheri za dunia na Akhera, basi kinai kutoka kwenye vilivyo mikononi mwa watu.” (4)
Njia ya kuing’oa tamaa
Njia ya kupambana na tamaa ni kukinai — kuridhika na kile ulicho nacho. Mtu anayejiridhisha na anachomiliki, hatakuwa na tamaa. Imam As-Sadiq (as) kwa ajili ya kuimarisha hisia ya kuridhika alisema:
«اُنْظُرْ إِلَی مَنْ هُوَ دُونَکَ وَ لاَ تَنْظُرْ إِلَی مَنْ هُوَ فَوْقَکَ.»
“Mtazame yule aliye chini yako, wala usimtazame aliye juu yako.” (5).
Naam, ikiwa mtu ataangalia wale walio chini yake katika mambo ya kidunia, basi hisia za shukrani, kuridhika na qana‘ah zitaimarika ndani yake. Kwa njia hii, tamaa na matamanio ya kupita kiasi yataangamizwa.
Lakini katika mambo ya kiroho na kimaadili, ni kinyume chake — mtu anapaswa kuwaangalia wale walio juu yake ili ajikite katika juhudi za kujikamilisha.
“Heshima iko katika kuridhika, na udhalili uko katika tamaa.
 Baki na heshima yako, usitafute udhalili.”
Rejea:
 1. Nahjul-Balagha, hekima ya 2
 2. Payam-e Imam Amir al-Mu’minin, juz. 12, uk. 31
 3. Surat as-Sajda, aya ya 17
 4. Bihar al-Anwar, juz. 70, uk. 168
 5. Mishkat al-Anwar fi Ghurar al-Akhbar, juz. 1, uk. 72
Imeandaliwa na: Kitengo cha Elimu na Utamaduni cha Shirika la Habari la Hawza.
 
             
                
Maoni yako