Kwa mujibu wa ripoti ya Kimataifa ya Shirika la Habari la Hawza, Roshan Abbasov, Mufti wa Urusi, katika Msikiti Mkuu wa Moscow, alikutana na wajumbe wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wakiongozwa na Rais wa Baraza la Jiji la Tehran, Bw. Mehdi Chamran.
Katika mkutano huu, manaibu wa Baraza la mamufti wa Urusi, Ildar Galiyev na Renat Abiyanov, pia walihudhuria.
Mufti Roshan alimfikishia Bw. Chamran salamu na ujumbe wa kiongozi wa kiroho wa Waislamu wa Urusi na akasisitiza mahusiano ya kirafiki ya ndani kati ya Urusi na Iran.
Alibainisha kuwa ziara nyingi rasmi za maafisa wa ngazi za juu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ndani ya Urusi daima zinaambatana na kuuzuru Msikiti Mkuu wa Moscow, jambo ambalo linaonesha uhusiano wa kiroho wa kina kati ya Moscow na Tehran.
Mufti Roshan Abbasov pia alirejelea ushirikiano na msaada wa Ubalozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Kituo chake cha Utamaduni katika nyanja mbalimbali za kidiplomasia, hasa katika miradi ya kimataifa kama vile Mkutano wa Viongozi wa Dini wa Nchi za BRICS, Mkutano wa Kimataifa wa “Njia ya Hariri ya Kiroho”, Tuzo ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu ya Nchi za BRICS na pia Mashindano ya Kimataifa ya Kusoma Qur’ani ya Moscow ambapo mshindi wake mwaka wa 2025 alikuwa mshiriki kutoka Iran.
Bw. Chamran, huku akishukuru kutokana na mapokezi muzuri, aliomba salamu zake za dhati afikishiwe Mufti Mkuu, Sheikh Ravil Gainutdin. Alipotaja ukuu na uzuri wa Msikiti Mkuu wa Moscow baada ya ukarabati wake mwaka wa 2015, alisisitiza kuwa katika ziara yake ya awali Moscow wakati wa Muungano wa Jamhuri za Sovieti, msikiti huu ulikuwa mdogo sana na ulikuwa mojawapo ya maeneo machache ya kidini nchini ambapo ibada iliruhusiwa kufanywa.
Mwishoni mwa mkutano huu, Mufti Roshan alimpa Bw. Chamran nakala moja ya albamu ya picha ya “Misikiti ya Urusi” iliyochapishwa na Machapisho ya “Chitai” kutokana na kuzuru kwake msikiti huu mkubwa na wa msingi wa Waislam wa Rusia.
 
             
                
Maoni yako