Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, jeshi la Yemen katika tamko muhimu lililotolewa limethibitisha taarifa ya kuuawa kishahidi kwa Jenerali Mohammad Abdulkarim al-Ghamari, Mkuu wa Majeshi ya Yemen.
Taarifa hiyo imesema kwamba: “Roho safi ya shahidi jenerali Mohammad al-Ghamari imepaa mbinguni akiwa miongoni mwa mashahidi wakubwa waliotangulia katika njia ya Beitul-Maqdis, akiwa anatekeleza jukumu lake la jihadi na dini.”
Taarifa hiyo imeendelea kusema kuwa: “Mapigano dhidi ya adui bado hayajakoma, na kwa msaada wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, adui wa Kizayuni atapata adhabu anayostahiki kwa jinai alizozifanya, hadi pale Quds itakapo kombolewa na utawala huo batili utakapofutwa kabisa.”
Jeshi la Yemen limesisitiza kwamba: “Njia tukufu iliyofuata na kuendelezwa na mashahidi wakubwa haitakoma kwa kuuawa kwa mmoja wao, bali ni njia ambayo vizazi vimeikubali na mashujaa wataiendeleza kizazi baada ya kizazi.”
Mwisho wa taarifa hiyo ilisema kwamba: “Kwa tukio hili, tunahuisha tena ahadi yetu ya uaminifu na kuendeleza kwa damu za mashahidi wakubwa.”
Maoni yako