Jumatano 29 Oktoba 2025 - 16:37
Wito wa kuonana na Malakuti ni heshima ya juu kabisa kwa mwanadamu/ kufunguliwa njia ya kuwa arif.

Hawza/ Mtukufu Ayatollah Jawadi Amuli amesisitiza: Qur’ani ni kitabu cha adabu na kinaonesha heshima kamili kwa mwanadamu. Mwenyezi Mungu anasema: (وَاتَّبِعُوا مِلَّةَ أَبِیکُمْ إِبْرَاهِیمَ), yaani nyinyi ni watoto wa Ibrahim Khalil na mnapaswa kuitambua heshima yenu.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Mtukufu Ayatollah Jawadi Amuli leo (Jumatano) katika somo la maadili katika Msikiti Mkuu wa Qom lililohudhuriwa na watu wa tabaka mbalimbali, aliendelea kufafanua maneno mafupi ya Nahjul Balagha, akirejea maneno yenye nuru ya Amirul Mu’minin (a.s) katika jumla ya 184 «مَا شَکَکْتُ فِی الْحَقِّ مُذْ أُرِیتُهُ» amesema:

Mtukufu amesema katika maneno haya: Wakati ukweli ulipooneshwa kwangu, sikuwahi kuwa na shaka juu yake tena.

Kauli hii ya Amirul Mu’minin inaonesha kuwa; maarifa ya kweli hupatikana kutokana na njia ya “kuoneshwa na kuona”, si kwa kusoma na kujadili tu; na kuona huku si kwa macho ya kawaida bali ni kwa macho ya moyo.


Alisisitiza kuwa: Mwanadamu kama anavyoipata elimu kupitia milango ya nje kama macho na masikio, anaweza pia kufikia ukweli kupitia milango ya ndani. Mwenyezi Mungu amemuwekea  mwanadamu shule mbili; moja ni shule ya nje ambayo njia yake iko wazi kwa wote na mtu hupata elimu ya nje kupitia masomo na utafiti katika chuo na taasisi, na nyingine ni shule ya ndani ambayo humpelekea kwenye ukweli kupitia kujitakasa nafsi, kuisafisha na kuitakasa. Kuunganisha njia hizi mbili, yaani elimu ya nje na uono wa ndani, kunawezekana na kunapendelewa.


Mtukufu huyo akaongezea: Mwanadamu ana aina mbili za kuona; kuona kwa hisia na kuona kwa moyo. Katika ulimwengu wa ndoto pia tunapitia uzoefu kwamba roho ya mwanadamu ina macho na masikio yake maalum. Kama vile elimu ya nje hupatikana kwa juhudi na kujifunza, maarifa ya ndani hupatikana kwa usafi na uangalizi wa macho, masikio na vitendo vya mwanadamu.
Akirejea mgawanyo wa maarifa kuwa “njia ya ufalme” na “njia ya Ufalme wa Mbingu” alisema: Masomo na uzoefu humfanya mtu kuwa mwanazuoni au faqihi, lakini njia ya ndani humfanya mtu kuwa arif na mwenye kuona. Si wote wanaofanikiwa kuona Ufalme wa Mbingu (Malakuti), lakini Mwenyezi Mungu ameifungua njia hiyo kwa wote; tunapaswa kujitahidi “kuiona”!


Mtukufu huyo akieleza kuwa Mwenyezi Mungu katika Qur’ani anazungumza na waja wake kwa adabu ya hali ya juu, akaongeza kusema: Qur’ani ni kitabu cha adabu na kinaonesha heshima kamili kwa mwanadamu. Mwenyezi Mungu alituambia: (وَاتَّبِعُوا مِلَّةَ أَبِیکُمْ إِبْرَاهِیمَ), yaani nyinyi ni watoto wa Ibrahim Khalil na mnapaswa kuitambua heshima yenu; hakuna utambulisho wa juu zaidi kuliko huu ambao Qur’ani imetutajia, Qur’ani imetuheshimu sana.


Hdhrat Ayatollah al-Udhma Jawadi Amuli aliendelea kwa kurejea aya tukufu isemayo (وَکَذَٰلِکَ نُرِی إِبْرَاهِیمَ مَلَکُوتَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ) akasema: Kama vile Mwenyezi Mungu alimuonesha Ibrahim (a.s) undani wa ulimwengu, watoto wa Ibrahim pia wameamrishwa kuutazama Ufalme wa Mbingu. Mwenyezi Mungu Mtukufu ametuambia: (أَوَلَمْ یَنْظُرُوا فِی مَلَکُوتِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ), yaani nyinyi pia angalieni, bali tazameni. Wito huu wa kuuona Ufalme wa Mbinguni ni heshima ya juu kabisa ya Mwenyezi Mungu kwa mwanadamu.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha