Kwa mujibu wa ripoti ya mwandishi wa shirika la habari la Hawza, somo la kila wiki la maadili la Ayatullah al-Udhma Subhani lilifanyika jioni ya Jumanne, huku likihudhuriwa na wanafunzi wa Hawza, wasomi na familia zao katika taasisi ya Imam Sadiq (a.s) mjini Pardisan Qom Iran.
Ayatullah Subhani aliashiria mafundisho ya Maimamu watoharifu (a.s), aliwataka wanafunzi vijana kutambua kina cha majukumu yao ya baadaye na kusisitiza kuwa elimu inapaswa kuwa yenye kumuokoa binadamu, kumsaidia na kurahisisha maisha, siyo elimu itayosababisha silaha za nyuklia na mauaji ya halaiki.
Kuwapa watoto hadhi ya utu
Mtukufu huyo alielezea mwenendo wa malezi ya Ahlul Bayt (a.s) na tukio la kukusanyika watoto wote wa Imam Hasan Mujtaba (a.s) pamoja na watoto wa kaka yake Imam Hussein bin Ali (a.s), na akasoma kauli ya kudumu ya Imam Hasan (a.s):
إنّکُم صِغارُ قَومٍ ویُوشِکُ أن تَکونوا کِبارَ قَومٍ آخَرینَ، فَتَعَلَّمُوا العِلمَ، فَمَن لم یَستَطِعْ مِنکُم أن یَحفَظَهُ فَلْیَکتُبْهُ ولیَضَعْهُ فی بَیتِهِ
"Nyinyi ni watoto wa jamii fulani na karibuni mtakuwa wakubwa wa jamii nyingine, basi jifunzeni elimu, na yule miongoni mwenu asiyeweza kuikumbuka, na aiandike na kuihifadhi nyumbani kwake."
Yeye aliwaambia wanafunzi: Ili kumwongoza mtu au kundi, lazima kwanza umpe hadhi na ukubwa wa utu wake. "Nyinyi ndio marjaa wa baadaye, wahadhiri wa vyuo vikuu vya baadaye... Kwa hiyo, tofauti na baba anayetoa nasaha kwa kumdhalilisha mtoto wake, lazima kwanza umkuze ili ajione kuwa mtu kamili wa baadaye, ndipo atakubali nasaha."
Uhitaji wa kuwekeza katika elimu kwa ajili ya baadaye
Baada ya kusisitiza juu ya utu, hoja ya pili ya Imam Hasan (a.s) kuhusu kujifunza elimu ilikuwa hii:
«…فَتَعَلَّمُوا الْعِلْمَ وَ حَفِّظُوهُ، وَ إِنْ لَمْ تَسْتَطِیعُوا أَنْ تَحْفَظُوهُ فَاکْتُبُوهُ».
"...Jifunzeni elimu na ihifadhini, na ikiwa hamuwezi kuikumbuka, basi iandikeni."
Mwanazuoni huyo aliendelea kusema: Watoto na kizazi kijacho watashika hatamu za nchi. Mtu asiye na elimu hawezi kuiendesha nchi. Kwa hiyo, mtaji wenu ni kusoma; siyo tu elimu ya dini. Iwe ni fiqhi, falsafa au hesabu. Mtaji huu unapaswa kuandaliwa tangia utotoni hadi ujanani. Ikiwa mtu ana kumbukumbu dhaifu, daima aandike na awe ni mwenye kurejea.
Ayatullah Subhani aliendelea kusisitiza umuhimu wa kuendelea na masomo na kuepuka uvivu, na kwa kusoma shairi la "al-Tughra'i":
حبُّ السلامةِ یُثْنی همَّ صاحِبه عن المعالی ویُغرِی المرءَ بالکَسلِ
"Kupenda raha humzuia mtu kufikia mambo makuu na humtia uvivu,"
Aliwaashiria watu wanaopenda raha na kuepuka taabu kuwa hawana azma: Wale wasiovumilia taabu daima ni wavivu na si watu wa kazi. Nyinyi mlio katika elimu, lazima mfanye kazi daima. Hata katika likizo rasmi za Hawza, kazi za kielimu zinapaswa kufanyika. Hata kama kwa mfano masomo yameahirishwa kwa ajili ya kumbukumbu ya shahada ya Bi Fatima (a.s), kutwalii na kazi za kielimu zisiahirishwe.
Ubora wa mwanazuoni na ujembe wa uokovu, ni sehemu inayoendana na uchamungu
Mtukufu huyo katika muendelezo wa mazungumzo yake, akiitaja hadithi tukufu isemayo:
«فَضلُ العالِمِ عَلَی العابِدِ کفَضلِ القَمَرِ عَلی سائرِ النُّجومِ لَیلَةَ البَدرِ»
"Ubora wa mwanazuoni juu ya mcha Mungu ni kama ubora wa mwezi juu ya nyota nyingine usiku wa mwezi mpevu,"
Alielezea ubora wa mwanazuoni, akielezea kisa cha mcha Mungu aliyekiacha aneo la ibada na kujiunga na shule, alisema kuwa kuwa; mwanazuoni lengo lake ni kuwaokoa wengine, wakati mcha Mungu anataka kujiokoa mwenyewe. Mcha Mungu anataka kuokoa zulia lake kutoka kwenye mawimbi, lakini mwanazuoni anajaribu kuiokoa dunia nzima. Manabii kwa sababu hii wana daraja za juu kwa kuwa walijitoa kwa ajili ya jamii.
Nyinyi mpo katika daraja ambayo Mungu amewapa ubora; kwa sababu hamjiokoi tu, bali mnaokoa wengine. Yeyote anayehutubu na kufundisha katika miji na vijiji, haokoi tu nafsi yake, bali anaokoa wote. Daraja hii kubwa hupatikana kwa kuwekeza katika ujana na kupata ukamilifu wa kielimu.
Kalamu ya mwanazuoni; huwaandaa mashahidi
Yeye alielezea nafasi ya kalamu katika kuendeleza mchakato wa uongofu, kwa kutaja hadithi maarufu isemayo:
«مِدَادُ الْعُلَمَاءِ أَفْضَلُ مِنْ دِمَاءِ الشُّهَدَاءِ»
"Wino wa wanazuoni ni bora kuliko damu ya mashahidi,"
Na akaelezea: Mwanzoni hadithi hii ni ngumu kukubaliwa kuwa kalamu ya mwanazuoni ina ubora juu ya damu ya shahidi, lakini ukweli ni kwamba shahidi anayekufa kwa ajili ya Mungu lazima awe amelelewa na mwanazuoni. Kama Sheikh Mufid, Sheikh Tusi na wanazuoni wakubwa wasingekuwepo na kuwalea mashahidi, shahidi huyo asingefikia daraja hiyo. Kwa hiyo, "midad al-ulama" yaani kujitolea kwa wanazuoni ambao huandaa watu, husababisha mashahidi kupatikana katika jamii.
Kumbukumbu ya siku za mwisho za maisha ya Ayatullah al-Udhma Borujerdi (r.a)
Mtukufu huyo baadae alisimulia kumbukumbu ya siku za mwisho za maisha ya Ayatullah al-Udhma Borujerdi (r.a) ambapo kwa kutegemea hadithi hiyo, alipata utulivu. Wakati hali yake haikuwa nzuri, kundi la wakubwa akiwemo Imam Khomeini, Ayatullah Golpayegani, Ayatullah Baha'uddini na wengine walikuwa naye. Yeye alisema:
"Laiti ningesimama dhidi ya suala la kuvuliwa hijabu na kufa shahidi. Naogopa mikono yangu kuwa mitupu huko akhera."
Marehemu Ayatullah Golpayegani alisema: «مِدَادُ الْعُلَمَاءِ أَفْضَلُ مِنْ دِمَاءِ الشُّهَدَاءِ» Yeye alijibu: "Ndiyo, hadithi hiyo ni sahihi." Ayatullah Golpayegani alisema: "Basi una nini cha kuhofia? Kama ungekuwa shahidi, mafanikio makubwa uliyopata katika uandishi na ufundishaji ungeyakosa." Na hapo Ayatullah al-Udhma Borujerdi alipata utulivu kidogo. Kwa kuandika kazi nyingi ikiwemo "Jami' Ahadith al-Shi'a" (midad al-ulama), alipata daraja ambayo kwa kufa shahidi katika suala la kuvuliwa hijabu, asingeipata.
Elimu yenye kuharibu, dhihirisho la ujinga wa kisasa
Ayatullah Subhani alitoa onyo kuhusu aina ya elimu inayotawala duniani na alisema: Pamoja na kutetea elimu, jihadharini; elimu inayopaswa kuenea ni ile ambayo itaiokoa jamii na kuipeleka kwenye daraja ya ubinadamu. Lakini elimu inayosababisha binadamu kuwaua binadamu wengine, kuanzisha vita na kufanya mauaji ya halaiki, haina thamani.
Mtukufu huyo alitumia maneno ya Imam Ali (a.s) katika Nahjul Balagha kuhusu zama za ujinga, na akaelezea hali ya sasa ya dunia: Kipindi cha jaahilia, chini ya mashati yao kulikuwa na hofu ya kila mmoja kwa mwenzake, na nguo yao ya nje ilikuwa silaha ya upanga. Ndani walikuwa na hofu, nje walikuwa na silaha. Hii ni alama ya ujinga.
Mwanazuoni huyo aliendelea kusema: Sasa ujinga umetawala Magharibi. Nchi zinaogopana na zinajihami. Mashindano haya ya silaha siyo ubinadamu. Hii siyo elimu. Elimu inapaswa kuwa ile inayo okoa uhai wa binadamu, inayosaidia na kurahisisha maisha, siyo elimu inayosababisha silaha za nyuklia na mauaji ya halaiki.
Ayatullah Subhani, ili kuzuia kudumaa katika njia ya elimu, aliashiria hadithi hii:
«مَنِ استَوی یَوماهُ فهُو مَغبونٌ، و مَن کانَ آخِرُ یَومَیهِ شَرَّهُما فهُو مَلعونٌ ، و مَن لم یَعرِفِ الزِّیادَةَ فی نفسِهِ فهُو فی نُقصانٍ ، و مَن کانَ إلی النُّقصانِ فالمَوتُ خَیرٌ لَهُ مِنَ الحیاةِ»
“Yeyote ambaye siku zake mbili ni sawa, basi amepotea; na yule ambaye mwisho wa siku yake ni mbaya kuliko mwanzo, basi amelaaniwa; na yule ambaye hajui ongezeko ndani ya nafsi yake, basi yuko katika upungufu; na yule aliye katika upungufu, basi kifo ni bora kwake kuliko maisha.”
Alieleza kuwa wanafunzi wanapaswa kufahamu kuwa kila siku isiyokuwa na tofauti na siku iliyotangulia ni kupoteza mtaji wa maisha yao. Hili ni jambo la wote, na kila mtu katika nafasi yoyote anapaswa kujitahidi kuhakikisha kuwa siku yake ya leo ni bora kuliko ya jana.
Maoni yako