Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjuma cha Shirika la Habari la Hawza Papa Leo katika hotuba yake ya Alhamisi alieleza umuhimu wa kuchapisha na kusambaza habari sahihi, hasa katika nyakati ambazo watu wengi hujali zaidi umaarufu wa habari kuliko ukweli wake. Avizitaka vyombo vya habari kote duniani kutokusaliti uaminifu wa kusambaza habari za kweli, hasa zile zinazohusu vita.
Papa aliirudia kwa uwazi wito wake wa awali na kusema: “Waandishi wa habari waliotekwa nyara na kuteswa wanapaswa kuachiliwa mara moja; katika sehemu yoyote ya dunia, kazi anayofanya mwandishi wa habari si kosa.”
Akaongeza kuwa: “Hii ni haki ambayo lazima ipiganiwe.” Kisha akawapa heshima maalumu waandishi wa habari mashahidi wa Ghaza.
Kuhusu hali ya sasa ambapo waandishi wa habari wanalazimishwa kubadilisha au kupotosha taarifa chini ya shinikizo, Papa aliieleza hali hiyo kuwa ni batili na isiyokubalika, akisisitiza kwamba uandishi wa habari ni taaluma inayopaswa kila wakati kuongozwa na ujuzi, uadilifu, na ujasiri.
Chanzo: Habari za Vatikani
Maoni yako