Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza, miongoni mwa masharti ya usahihi wa wudhu na josho katika hukumu za twahara ni kwamba maji yafike katika sehemu zote za nje ya mwili (ngozi), hivyo basi, chochote kinachokuwa kizuizi cha nje kati ya maji na ngozi, endapo kuondoa kwake kunawezekana ni lazima kuondolewa, kikiwa bado kimebaki kinaweza kusababisha twahara hiyo kubatilika.
Masuala yanayohusiana na tatoo, ambayo yamekuwa jambo la kawaida katika zama hizi, ni miongoni mwa mambo yanayoulizwa sana kuhusu athari yake katika usahihi wa wudhu na josho, hukumu ya kisheria katika jambo hili inategemea moja kwa moja iwapo tatoo inahesabiwa kuwa ni kizuizi katiks kufika maji kwenye ngozi au la.
Mtukufu Ayatullah Khamenei ametoa majibu ya kisheria katika istiftaa hii ambayo tunaiwasilisha kwenu kama ifuatavyo:
Swali:
Je, kutawadha au kuoga janaba huku kukiwa na tatoo ni sahihi?
Jawabu:
Iwapo tatoo ni rangi tu, au ipo chini ya ngozi na juu ya ngozi hakuna kitu kinachozuia maji kufika, basi wudhu na josho ni sahihi.
Chanzo: www.leader.ir
Maoni yako