Jumapili 31 Agosti 2025 - 00:36
Tunataka Wa-Iraq waliokamatwa Saudi Arabia waachiwe huru

Hawzah/ Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Sadruddin Qubanchi alisema: makumi ya Wairaqi wamekuwa wakishikiliwa katika magereza ya Saudi Arabia kwa zaidi ya mwaka mmoja, baadhi yao, kosa lao lililotangazwa na Saudi Arabia ni kuinua bendera ya Hashd al-Shaabi

Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjuma cha Shirika la Habari la Hawza, Sayyid Sadruddin Qubanchi, Imamu wa Ijumaa wa Najaf Ashraf, katika khutba za Ijumaa alizozitoa katika Husseiniyya Azam Fatimiyya ya Najaf Ashraf, alisema: Idara ya Awqaf ya Kishia imewasilisha mpango bungeni ikidai kupitishwa kwa muswada wa hukumu za kisheria za Ja’fari ndani ya siku 30 ili utekelezwe, hii ni hatua chanya na tunatarajia kwamba itapigiwa kura.

Aliongeza kuwa: Hapa napenda kutoa shukrani na pongezi kwa Idara ya Awqaf na Bunge la Wawakilishi.

Katika sehemu nyingine ya khutba, Qubanchi alisema: Makumi ya Wairaqi wamekuwa wakishikiliwa Saudi Arabia kwa zaidi ya mwaka mmoja, baadhi yao kosa lao lilitangazwa kuwa ni kuinua bendera ya Hashd al-Shaabi, Wizara ya Mambo ya Nje ya Iraq kwa sasa imeingilia kati ili kuwaachia huru.

Akaongeza kuwa: Tunataka kwamba ikiwa ni kweli wamekosea, warejeshwe katika mahakama ya Iraq, na iwapo hakuna kosa lililothibitishwa dhidi yao, basi waachiwe huru.

Imamu wa Ijumaa wa Najaf Ashraf, katika sehemu nyingine ya khutba yake alisema: Wiki hii mgombea mmoja wa Kiamerika alichoma moto Qur’ani Tukufu mbele ya hadhira ya kimataifa na akatangaza: “Nitaufuta Uislamu.” Hakuna mtu aliyeukemea uhalifu huu.

Aliendelea kusema: Tunaamini kwamba kitendo hiki ni tangazo la vita vya kimaadili na kiutamaduni dhidi ya Uislamu, ni dalili ya kushindwa na hisia kwamba Uislamu ni ustaarabu mbadala unaokuja duniani.

Kuhusu Ghaza, Hujjatul-Islam Qubanchi alisema: Israel, kwa msaada wa nguvu kubwa za dunia, imetishia kuivamia Ghaza, tunaamini kuwa huu ni uvamizi dhidi ya ulimwengu wa Kiislamu na uvunjaji wa makubaliano ya usitishaji vita.

Katika khutba ya kidini, aligusia kumbukumbu ya shahada ya Imam Hasan Askariy (a.s.) katika siku ya 8 Rabiul-Awwal, siku ambayo pia ghaiba ya Imam wetu al-Muntadhar (a.s.) ilianza mwaka 260 Hijria. Katika uhusiano huu alelezea maswali matatu:

1. Kwa nini kuna ghaiba?
2. Je, jambo hili linawezekana?
3. Imam yupo wapi?

Alisema: Majibu ya maswali haya yameelezwa na Maimamu (a.s.).

Kuhusu swali la kwanza, Imam Hasan Askariy (a.s.) alimwandikia Sheikh Mufid barua akisema: “Japokuwa tumekaa katika sehemu iliyo mbali na maskani ya madhalimu – kwa mujibu wa hekima aliyoonesha Mwenyezi Mungu kwetu na kwa wafuasi wetu waaminifu, maadamu dola ipo mikononi mwa waovu.”

Kuhusu swali la pili, alisema: Jibu ni ndio – kama Qur’ani ilivyosema kuhusu Nabii Isa bin Maryam (a.s.): “Bali Mwenyezi Mungu alimnyanyua kwake.” (Qur’ani). Hivyo nguvu za Mwenyezi Mungu Mtukufu ziko juu ya mambo yote.

Ama swali la tatu, Imam yuko wapi? Jibu ni kwamba yeye yupo pamoja nasi, lakini sisi hatumuoni.

Aliendelea: Swali la mwisho ni: Wajibu wetu katika zama za ghaiba ni upi? Jibu limeelezwa na Maimamu wetu (a.s.) kuhusu nafasi na majukumu yetu, kama alivyosema Imam Hasan Askariy (a.s.): “Hakuna udhuru kwa yoyote kati ya wafuasi wetu katika kutia shaka juu ya yale ambayo watu wetu waaminifu wanayapokea kutoka kwetu.” Wao ni wanazuoni wanaojua dini na hukumu zake; hivyo hairuhusiwi kuwatilia shaka.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha