Kwa mujibu wa ripoti ya idara ya kimataifa ya Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah A‘rafi alikutana na kundi la walimu, wanazuoni Waislamu na wafuasi wa Ahlul-Bayt (a.s.) nchini Malaysia.
Katika kikao hicho, Ayatullah A‘rafi, sambamba na kutoa pongezi za maadhimisho ya miaka 1500 ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (s.a.w.), alieleza sifa za Mtume Mtukufu zilizomo katika Nahjul-Balagha, na akaeleza kuwa Nahjul-Balagha ni miongoni mwa vyanzo bora kabisa kwa ajili ya kumtambua na kumweleza Mtume wa Uislamu.
Mkurugenzi wa hawza nchini Iran alisema: Amirul-Mu’minin (a.s.) alieleza zaidi ya sifa mia moja kuhusu Mtume wa Uislamu, na miongoni mwa hizo ni “utumwa na ibada ya Mtume kwa Mwenyezi Mungu”, “utume mahsusi kutoka kwa Allah”, “khatamiyya ya Mtume (yaani kuwa Mtume wa mwisho)”, “kuwafungulia binadamu njia zilizokuwa zimefungika katika historia”, “kubainisha haki kwa mbinu sahihi”, “kuangamiza majeshi ya batili”, “kuvunja fahari na vitisho vya uongo”, na “kubeba amana ya Mwenyezi Mungu.”
Mjumbe wa Baraza Kuu la Hawza aliwapa wosia wapenzi wa Ahlul-Bayt (a.s.) na walimu waliokuwepo katika kikao hicho, akasisitiza umuhimu wa kulinda usalama, uhuru, umoja na heshima ya Malaysia na ulimwengu wa Kiislamu, pia aliwataka wawe wachangiaji wa kuimarisha uhusiano kati ya serikali za Kiislamu hususan Iran na Malaysia katika nyanja mbalimbali.
Aidha, alisisitiza juu ya mwelekeo wa kujenga utambulisho wa kistaarabu na wa umma wa Kiislamu, na kuepuka misimamo ya kupetuka mipaka na mitazamo ya makundi makundi, Alisema: “Msimamo wa Ahlul-Bayt (a.s.) ni msimamo wa hikma, busara, umoja na utambulisho wa Kiislamu wa pamoja.”
Ayatullah A‘rafi alibainisha kuwa msimamo wa Jamhuri ya Kiislamu baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ni wa madhehebu tofautu na unaozingatia maslahi ya umma wa Kiislamu, na hasa katika kuilinda Palestina na taifa madhulumu la Ghaza, jambo ambalo ni sehemu ya siasa thabiti ya mfumo wa Kiislamu, aidha, alisema kuwa: “Maneno ya Ahlul-Bayt (a.s.) ypo juu ya dhehebu moja au utamaduni mmoja, bali ni manebo ya ulimwengu mzima na ya kibinadamu kwa ajili ya kupata furaha ya wanadamu wote.”
Kisha akazitaja shakhsia kama vile Imam Khomeini, Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Shahid Sadr na Shahid Mutahhari kuwa ni miongoni mwa wanazuoni wa kweli wa zama hizi waliokuwa wamenufaika na maneno ya Ahlul-Bayt (a.s.).
Maoni yako