Jumapili 31 Agosti 2025 - 17:03
Al-Wala’i: Kupata Shahada viongozi wa Yemen ni Sanadi ya utiifu wa taifa hili kwa dhamira ya Palestina

Hawza/ Katibu Mkuu wa Kataib Sayyid al-Shuhada, ameeleza kuwa kuuawa kishahidi kwa viongozi wa Yemen katika shambulio la hivi karibuni lililofanywa na utawala wa Kizayuni ni ushahidi wa utiifu wa taifa hilo kwa dhamira ya Palestina na kupambana na dhulma, na ni alama iliyo wazi ya msimamo thabiti wa Wayemen

Kwa mujibu wa ripoti ya idara ya kimataifa ya Shirika la Habari la Hawza, Katibu Mkuu wa “Kataib Sayyid al-Shuhada” kupitia ujumbe aliouchapisha kwenye mtandao wa kijamii X, ametuma salamu za rambirambi kwa kuuawa kishahidi kwa Waziri Mkuu na baadhi ya mawaziri wa serikali ya Yemen katika shambulio la hivi karibuni lililofanywa na utawala wa Kizayuni, na akalieleza jambo hilo kuwa ni alama ya wazi ya msimamo thabiti wa Wayemen katika kuilinda Palestina na kupambana na dhulma.

Abu Alaa al-Wala’i, akiheshimu nafasi ya taifa la Yemen chini ya uongozi wa Sayyid Abdul-Malik Badruddin al-Houthi, alisisitiza: “Wayemen wamesimama katika ngazi za juu kabisa ya heshima, mshikamano na mapambano, wakiwa bega kwa bega na taifa madhulumu la Palestina na watu wa Ghaza waliozingirwa.”

Ameshutumu shambulio la hivi karibuni la Wazayuni kama “jinai dhalimu na ya uoga” na akaongeza: “Damu safi za viongozi wa Yemen zimeudhihirishia tena ulimwengu uthabiti na uhalisia wa misimamo ya taifa hili katika kuwatetea wanyonge.”

Katibu Mkuu wa Kataib Sayyid al-Shuhada pia amelishutumu jeshi la Kizayuni kwa “unyama na kupuuzia waziwazi thamani za kibinadamu na sheria za kimataifa”, na akabainisha: “Wayemen kwa ushujaa wamesimama dhidi ya adui, na wataendelea kubaki pamoja na watu wa Palestina.”

Al-Wala’i mwishoni ameheshimu hadhi ya mashahidi na kuomba dua kwa ajili ya kupona kwa majeruhi, akasisitiza: “Mashahidi hawa watadumisha zaidi azma ya jengo la muqawama katika kuwatetea wanyonge.”

Inapaswa kusemwa kuwa katika shambulio la siku ya Alhamisi lililofanywa na ndege za kivita za Israel mjini Sanaa, mji mkuu wa Yemen, “Ahmad Ghalib al-Rahwi” Waziri Mkuu na idadi ya mawaziri waliuawa.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha