Jumapili 31 Agosti 2025 - 20:50
Hizbullah: Uvamizi wa kinyama dhidi ya Yemen ni jinai mpya iliyoongezwa kwenye jalada la jinai za Wazayuni

Hawza/ Hizbullah katika tamko lake imetoa rambirambi zake za dhati na pole za kina kwa taifa ndugu la Yemen na uongozi wake wa mapambano chini ya uongozi wa Sayyid Abdulmalik Badruddin Al-Houthi

Kwa mujibu wa taarifa ya Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, Hizbullah katika tamko lake imetoa rambirambi zake za kina na pole zake za dhati kwa taifa ndugu la Yemen na uongozi wake wa mapambano chini ya uongozi wa Sayyid Abdulmalik Badruddin Al-Houthi, kutokana na kuuwawa kishahidi kwa Mujahid Ahmad Ghalib Al-Rahwi, Waziri Mkuu wa Serikali ya Mabadiliko na Ujenzi, pamoja na kundi la mawaziri, kufuatia uvamizi wa kihaini na wa kiwoga wa Kizayuni uliolenga kikao rasmi kisicho cha kijeshi cha Serikali ya Yemen mjini San-aa.

Hizbullah imeashiria kwamba uvamizi huu wa kinyama si chochote ila ni jinai mpya iliyoongezwa kwenye jalada la jinai za Wazayuni, ambazo zimeenea kuanzia Gaza, Lebanon, Syria, Yemen na Iran, na ambazo zimeongewa katika damu ya watoto, wanawake, wazee na raia wasio na ulinzi.

Hizbullah imeongeza kusema: Jinai hii inadhihirisha hakika ya adui huyu ambaye ametenda jinai za kutisha zaidi katika historia, ametekeleza mauaji ya halaiki na kulazimisha taifa zima kuangamia kwa njaa huku ulimwengu ukishuhudia.

Hizbullah imesisitiza kwamba uwepo thabiti na wenye nguvu wa Yemen katika uwanja wa kuutetea mradi wa Palestina, licha ya uvamizi na mzingiro unaolikabili, ni mfano wa kweli na wenye uaminifu zaidi pamoja na subira na uthabiti, hii ni heshima na fahari kubwa kwamba katika wakati ambapo ulimwengu mzima umenyamaza na umekosa kujali, na hauwezi kutoa msaada wowote au kuchukua msimamo dhidi ya mauaji ya halaiki yanayotekelezwa na utawala wa Kizayuni, Yemen injitolea makubwa kwa ajili ya kuisaidia Ghaza na kuitoa kwenye vizuizi.

Mwisho wa tamko lake, Hizbullah imesisitiza: Tuna yakini kwamba uvamizi huu utazidisha tu azma, irada na uthabiti wa taifa la Yemen, na hautazuwia uongozi wao jasiri kuendelea kushikamana na msimamo wao wa kimsingi wa kuisaidia Ghaza na watu wake wa mapambano. Damu ya viongozi hawa mashahidi wema itakuwa laana kwa utawala wa Kizayuni na ishara ya uthabiti na mapambano.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha