Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza, Ayatollah Mohsen Araki, mjumbe wa Baraza Kuu la Hawza, katika mkutano na Baraza la wananchi la kampeni ya “Sauti ya Ghaza” alisisitiza: Kazi ambayo mmechukua ni jukumu la kisheria la dharura na la lazima; kwa kuwa “nafsi na mali za Waislamu” ziko katika hatari ya kuteketezwa.
Mjumbe wa kamati ya Baraza la Wataalamu wa Uongozi, huku akionyesha imani kamili kwa wanaharakati wa kampeni hiyo, aliongeza kwa kusema: Nina imani na kundi hili lote, sisi, kwa kadiri ya uwezo tulionao, tupo tayari kutoa huduma usiku na mchana.
Yeye aliihesabu harakati hii kuwa ni miongoni mwa “wajibu ulio wajibu zaidi (اوْجَبُ الْواجِباتِ)” na akasisitiza: Watu wote lazima watumie uwezo wao wote katika kuiunga mkono hatua hii.
Mjumbe wa Baraza Kuu la Hawza huku akisisitiza juu ya ulazima wa kuzidisha misaada alisema: Hatupaswi kujizuia, bali nguvu zote nchini Iran, Iraq na nchi za ukanda huu lazima zisimame mstari wa mbele.
Ayatollah Araki alibainisha: Kazi hii ni jukumu la kimungu na ni lazima tuwe na majibu mbele ya Mwenyezi Mungu; natumai wapenzi wote wenye uchungu watafika kwa haraka ili kuwasaidia.
Ni lazima ieleweke kuwa, kampeni ya “Sauti ya Ghaza” imeundwa kwa lengo la kuvunja kuzingirwa watu wa Ghaza na kuimarisha harakati ya misafara ya meli zinazoelekea katika pwani hiyo, na inasubiri kwa hamu wapenzi wote wa Kiirani wenye ghera wanaotaka kushirikiana na kusaidia katika jambo hili muhimu.
Maoni yako