Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Bwana Kolbni, katika safari yake ya kutembelea Jordan, alizindua mpango huu na kutangaza kuwa kwa ajili ya kuwaunga mkono watu wa Ghaza na Palestina, kwa namna ya kimaonyesho, miji ya Palestina inatangazwa kuwa eneo la kumi na moja la Barcelona.
Barcelona hapo awali, baada ya mauaji ya halaiki ya Waislamu nchini Bosnia na Herzegovina, ilitangaza mji wa Sarajevo, ambao ni mji mkuu wa Bosnia, kuwa eneo lake la kumi na moja, ili kuwaunga mkono Waislamu wanyonge wa Bosnia na Herzegovina na kuwasaidia kurejesha hali zao.
Kolbni alisema: “Hatua hii si hotuba ya kawaida wala kauli za kishabiki, bali ni msaada wa kweli kwa Ghaza, Sisi katika manispaa tuna mpango wa kuwa na msaada wa kudumu kwa wakimbizi wa Kipalestina.”
Chanzo: Shirika la Habari la Anadolu
Maoni yako