Ijumaa 29 Agosti 2025 - 00:19
Sheria ya Hashd al-Shaabi imecheleweshwa kati ya shinikizo la kimataifa na migawanyiko ya ndani na bunge lililo chini ya utawala

Hawza/ Katikati ya mazingira ya kisiasa yaliyojaa vurugu na mgawanyiko, sheria ya kuratibu vikosi vya Hashd al-Shaabi, moja ya sheria muhimu za kiserikali na kiusalama, bado imesalia kusimama bungeni

Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjuma cha Shirika la Habari la Hawza, licha ya umuhimu wake kama moja ya sheria kuu zenye sura ya kiserikali na kiusalama, sheria ya kuratibu vikosi vya Hashd al-Shaabi — ambayo inakusudia kuratibu kazi za vikosi hivyo na kuhakikisha haki za wapiganaji wake — imegeuka kuwa kitovu cha migongano ya ndani na shinikizo la kigeni, na kufanya kupitishwa kwake kuwa jukumu lenye hofu kwa nguvu za kisiasa za Iraq.

Wakati wananchi wanatarajia kutendewa haki wapiganaji wa Hashd al-Shaabi waliokuwa na nafasi ya msingi katika kupambana na ugaidi, tuhuma zimezidi kuongezeka kwamba ajenda za kimataifa na maslahi ya vyama vya kisiasa ndiyo kikwazo cha kupitishwa kwa sheria hiyo.

Jha, mbunge wa Iraq, alieleza katika mahojiano kwamba sheria ya Hashd al-Shaabi imeandaliwa kimsingi ili kuratibu kazi ya taasisi hiyo na kusawazisha mambo ya kiutawala na kisheria ya wapiganaji wake, lakini kupitishwa kwake kumezuiliwa na ukuta wa shinikizo la kimataifa linaloelekezwa dhidi ya Iraq.

Alibainisha pia kwamba kuna mahesabu ya kisiasa ya ndani yanayohusiana na misimamo na maslahi ya vyama, jambo lililofanya baadhi ya vyama — licha ya umuhimu wa Hashd al-Shaabi kwa usalama wa taifa — kusimama kinyume chake.

Al-Yasiri aliongeza kuwa sheria hiyo imekumbwa na upinzani na tofauti za maoni miongoni mwa makundi ya kisiasa mbalimbali, yakiwemo Wasunni, Wakurdi na hata baadhi ya makundi ya Kishia, yaliyogawanyika kati ya wanaounga mkono na wanaopinga, hali hiyo imezuia kupatikana msimamo wa pamoja kuhusu kupitishwa kwake.

Kwa upande mwingine, Ibrahim al-Sarraj, mchambuzi wa kisiasa wa Iraq, alisema kuwa bunge la Iraq limekuwa likijisalimisha zaidi kwa maslahi binafsi na shinikizo la kigeni, kiasi cha kushindwa kupitisha sheria muhimu za kitaifa.

Al-Sarraj aliongeza pia: “Shinikizo la Marekani lina nafasi kuu katika kuzuia kupitishwa kwa sheria ya Hashd al-Shaabi, huku ikijitahidi kupitisha makubaliano yenye utata kama makubaliano ya uwekezaji na Saudi Arabia, jambo linaloonesha aina nyingine ya udhibiti dhidi ya uwezo wa kiuchumi wa Iraq.”

Mchambuzi huyo alibainisha pia kuwa kikao cha hivi karibuni cha upigaji kura kuhusu orodha ya mabalozi kilikuwa kinyume cha katiba, kwa kuwa kilifanyika bila ya kuwepo idadi ya kutosha ya wajumbe na bila wasifu wa wagombea kusomwa, hili linaonesha mwelekeo wa baadhi ya makundi kusukuma mbele nyuso zenye utata kwa msingi wa makubaliano finyu ya kisiasa.

Alieleza zaidi kwamba uongozi wa bunge, pamoja na baadhi ya vikosi, unalenga kupitisha makubaliano yatakayoiweka Iraq katika minyororo yao kwa miongo kadhaa, pengine zaidi ya miaka hamsini.

Inafaa kutajwa kuwa; bunge la Iraq hivi karibuni limekumbwa na machafuko ya kisiasa yaliyoongezeka kutokana na mivutano juu ya sheria muhimu kama sheria ya Hashd al-Shaabi, huku wananchi wakikabiliwa na migogoro inayoongezeka ya kiuchumi na huduma, hali hii imezidisha ukosoaji wa wananchi dhidi ya taasisi ya kisheria ambayo, kwa mujibu wa wachambuzi, inatii zaidi shinikizo la kigeni kuliko mahitaji ya maslahi ya taifa.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha