Kwa mujibu wa ripoti ya Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Sadruddin Qubanchi, Imamu wa Ijumaa wa Najafu Ashraf, katika khutba za Sala ya Ijumaa alizoitoa katika Huseinia kubwa ya Fatimiyya Najafu Ashraf, alisema: “Mada moto ya Iraq leo hii ni kuhusu vikosi vya Basiji ya Wananchi (Hashd al-Sha‘bi), ambapo pambano ni juu ya kuvunjwa kwao, sisi tunaamini kwamba Hashd al-Sha‘bi ni nukta ya nguvu ya Iraq, na Hashd al-Sha‘bi ni nembo ya heshima na fahari ya Iraq, kuvunjwa kwa Hashd al-Sha‘bi ni sawa na kukata mkono wenye nguvu wa Iraq, kwa kuwa mkono huo ndio uliosimamisha kusonga mbele kwa Daesh.”
Katika sehemu nyingine ya khutba yake alisema: “Wizara ya Utamaduni ya Iraq kwa mnasaba wa siku ya Arubaini ya Imam Husein (a.s) iliandaa tamasha la ‘Wimbo wa Huseini’.”
Imamu wa Ijumaa Najafu Ashraf alisema: “Tunashukuru kwa hatua hii ya ukarimu ya wizara, lakini Mwenyezi Mungu atiiwi sehemu ambayo anaasiwa; kwani tamasha hili lilihusisha muziki na mapambo ya wanawake, Je, Imam Husein (a.s) angelikubali jambo hili?”
Aliendelea kusrna: “Imam Husein (a.s) ni darasa na maadili, si wimbo na upotovu wa wanawake, kwa hivyo, tunataka majlisi za Huseini zisafishwe na kuondolewa upotovu wa kidini na kimaadili.”
Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Sadruddin Qubanchi kuhusu kauli za baadhi ya wanasiasa alisema: “Kauli imetolewa na baadhi ya wanasiasa wenye ushawishi kwamba Mashia hawana uwezo wa kuongoza dola, bali wapo tu kwa ajili ya kupiga vifua, siyo kwa ajili ya kuongoza serikali.”
Alisema: “Sisi tunasema Mashia ndio wa kwanza waliouamini mradi wa ushiriki wa kisiasa, Mashia ndio waliouangamiza ugaidi wa Daesh, Mashia ndio waliouzima mradi wa kuigawa Iraq, utulivu na usalama ndiyo ushahidi bora wa mafanikio ya serikali ya Kishia, na ziara za mamilioni ndizo uthibitisho bora zaidi wa jambo hili, kwa hivyo, tunawaomba waache kutumia lugha ya mfarakano.”
Imamu wa Ijumaa Najafu Ashraf kuhusu kuondoka kwa wanajeshi wa Marekani kutoka Iraq alisema: “Kuondoka kwa vikosi vya muungano wa kimataifa kutoka Iraq kunaanza mwezi huu, na kunatarajiwa kukamilika kufikia mwisho wa mwaka 2026.”
Aliongeza kwa kusema: “Tunaamini kwamba hii ni hatua katika njia sahihi, na Iraq ina uwezo wa kudumisha nafasi yake ya ndani na ya kimataifa.”
Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Sadruddin Qubanchi kuhusu janga la “al-Khassfah” alisema: “Janga la Khassfah, ambapo kaburi la pamoja limepatikana katika eneo la Khassfah huko Mosul, likiwa na miili 20,000 ya watu waliouawa na Daesh.”
Aliendelea kusema: “Idara Kuu ya Makaburi ya Pamoja imetangaza kwamba katika siku moja na katika mauaji ya kimbari, miili ya wanaume 2,000 waliouawa kwa kunyongwa imepatikana, Je, msimamo wa dunia ya kibinadamu uko wapi? Huu ndio uhalifu ambao Daesh walifanya Iraq, na huyu mwanachama wa Daesh, al-Jawlani, sasa amekuwa kiongozi wa dola bila ya kuadhibiwa.”
Khatibu wa Ijumaa Najafu Ashraf katika khutba ya kidini aligusia kumbukumbu ya kifo cha Mtume Mtukufu wa Uislamu (s.a.w.w) na kusema: “Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema katika Qur’an Tukufu:
«وَلَوْ أَنَّهُمْ إِذْ ظَلَمُوا أَنْفُسَهُمْ جَاءُوکَ فَاسْتَغْفَرُوا اللَّهَ وَاسْتَغْفَرَ لَهُمُ الرَّسُولُ لَوَجَدُوا اللَّهَ تَوَّابًا رَحِیمًا»Na lau pale walipo jidhulumu nafsi zao wangeli kujia, wakamwomba Mwenyezi Mungu msamaha, na Mtume akawaombea msamaha, hapana shaka wangeli mkuta Mwenyezi Mungu ni Mwenye kupokea toba na Mwenye kurehemu.”
Aliongeza kwa kusema: “Kwa msingi huo, Mtume (s.a.w.w) anasema: ‘Nimehifadhi shafa‘a yangu kwa ajili ya wakosefu wakubwa katika umma wangu.’”
mamu wa Ijumaa Najafu Ashraf pia alikumbusha baadhi ya maadili ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) ambayo yameidhinishwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kisema:
«وَإِنَّکَ لَعَلی خُلُقٍ عَظیمٍ»
(Na kwa yakini wewe una tabia njema na tukufu mno).
Maoni yako