Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, maandamano na mgomo huu wa kula umefanyika kwa lengo la kuwaunga mkono Wapalestina wanaokabiliwa na mashambulizi ya Israel na pia kupinga kuzorota zaidi kwa hali ya Ghaza, na kwa hakika umeitishwa kufuatia wito wa mashirika yasiyo ya kiserikali.
Kundi la uratibu wa harakati hii kubwa linaundwa na idadi ya madaktari ambao wamewasilisha madai mbalimbali, ambapo madai makuu ni kusitisha sera ya njaa ya kimfumo inayoendelezwa Ghaza kwa ajili ya mauaji ya halaiki.
Mgomo wa kula huu ni ishara ya kusisitiza ongezeko la wasiwasi, hasa miongoni mwa wafanyakazi wa sekta ya afya nchini Morocco, kuhusiana na hali mbaya kupita kiasi iliyosababishwa na Israel dhalimu huko Ghaza.
Hospitali na vituo vingi vya afya vya Ghaza vimeharibiwa kabisa kutokana na mabomu ya utawala katili wa Kizayuni, jambo linalofanya utoaji wa huduma bora za kitabibu na matibabu kuwa jambo lisilowezekana.
Shirika la Afya Duniani limeripoti kwamba trakriban asilimia 94 ya hospitali za Ghaza zimeharibiwa.
Kitendo cha madaktari wa Morocco ni miongoni mwa harakati kubwa kadhaa duniani kote zinazofanyika kwa ajili ya kuwaunga mkono watu wanyonge wa Ghaza.
Chanzo: Morocco World News
Maoni yako