Kwa mujibu wa idara ya kimataifa ya Shirika la Habari la Hawza, katika kukaribia hatua ya kihistoria kwenye maisha ya mwanadamu, dunia imo katika hali nyeti ambapo wanadamu waliomakinika kutoka tamaduni zote duniani wametambua mabadiliko haya. Hatua ambayo ndani yake vita ya mwisho kati ya ustaarabu wa kibinadamu unaopigania uhuru na ustaarabu wa kiunyama imeanza.
Katika njia hii yenye kuamua hatima, kampeni ya “Imam Mahdi ni nani?" katika Arbaeen ya mwaka huu, inalenga kuwaandaa wanadamu kwa ajili ya mapambano haya makubwa, na inafanya kazi katika vituo vinne muhimu vilivyoko kwenye njia ya matembezi ya Arbaeen.
Kwa mujibu wa ripoti hii, vituo vya kampeni katika Arbaeen ya mwaka 1447 Hijria, vinakusanya:
Najaf / mwanzoni mwa barabara ya Imam Swadiq (as) – kituo kikuu cha kampeni, nguzo 952 / kitengo cha kimataifa, uwanja wa ndege wa Imam Khomeini (r.a) Tehran / jengo la Salaam, na uwanja wa ndege wa Shahid Hashimi Nejad mjini Mashhad.
Kampeni hii, katika mwelekeo wa kutimiza malengo ya kimungu na kuwaandaa wanadamu kwa ajili ya kuingia katika mustakabali uliojaa nuru na ahadi ya mwokozi, inatoa maelezo kuhusu maeneo matatu muhimu ambayo ni ya lazima kwa ajili ya kuchangia katika ustaarabu wa kimataifa wa baadaye, miongoni mwa maeneo hayo ni:
1. Kufahamu wakati na kuchambua historia ya mwanadamu – kuelewa hatua ya sasa ya historia na kuchagua upande sahihi kwa ajili ya mustakabali.
2. Marekebisho ya mtindo wa maisha na kulinda nguvu za kimwili – kujiandaa kushiriki kwa ufanisi katika ustaarabu wa baadaye wa kimataifa.
3. Kujua zana za ghaibu na ‘ngao za nuru’ – kutumia mafundisho ya "Sahifa Sajjadiyya" kwa ajili ya kuwalinda wanadamu dhidi ya matatizo ya zama za mwisho.
Aidha, shughuli hizi hazisaidii tu kuimarisha imani ya mtu binafsi na ya kijamii, bali pia zinawaandaa watu kukabiliana na changamoto na misukosuko ya kimataifa katika njia hii, wanadamu wote wanakaribishwa kukua na kufikia ukamilifu kwa pamoja ili kujiandaa kwa ajili ya mustakabali uliojaa nuru na matumaini.
Katika muktadha huo, maudhui ya kielimu yanatolewa kwa mazuwari. Miongoni mwa vitabu hivyo ni:
“Nguzo 14 za Nuru katika Zama za Mwisho” – dua 14 muhimu kwa ajili ya kukabiliana na matatizo ya zama za mwisho.
“Kila Kitu Kuhusu Vita vya Mwisho wa Zama” – utambulisho wa mafundisho muhimu kuhusu vita ya ustaarabu na nafasi ya mazuwari katika mapambano ya mwisho.
“Njoo Uchukue Suluhisho la Tatizo Lako” – warsha za mafunzo kwa ajili ya kutatua matatizo ya mtu binafsi na ya kijamii.
“Mbinu za Kuilinda Nafsi katika Zama za Mwisho” – utambulisho wa dua 20 za kinga kutoka katika "Sahifa Sajjadiyya" kwa ajili ya kuimarisha ustahimilivu wa kiroho.
Taasisi ya "Muntadhirān al-Munjī" imejitahidi kuhakikisha kwamba katika Arbaeen hii, mazuwari wa Imam Hussein (as), pamoja na matembezi, washiriki pia katika kusambaza maudhui ya kielimu kuhusu kujiifahamu na kinga za zama za mwisho. Kwa ajili hiyo, maudhui mbalimbali na zenye mvuto zinatolewa kwa lugha tatu: Kifarsi, Kiingereza, na Kiarabu katika vituo vinne vya kampeni, ili kuwafikia wadau wake.
Kwa hakika, maudhui haya yanaweza kuwa na nafasi muhimu katika kuwaandaa watu kwa ajili ya kukabiliana na misukosuko na changamoto za kimataifa.
Wale wanaopenda kupata taarifa zaidi na kupakua maudhui ya kampeni, wanaweza kutembelea tovuti: "WhoisImamMahdi.com"
Mwisho wa taarifa.
Maoni yako