Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatollah Alireza A'rafi, katika hotuba ya Swala ya Ijumaa ya tarehe 17 Mordaad 1404 (kwa mujibu wa kalenda ya Shamsiya), iliyofanyika katika Muswalla wa Quds, Qom, sambamba na kutoa pongezi kwa mnasaba wa Siku ya Mwandishi wa Habari, alisema: Tunaitukuza kumbukumbu ya shahidi Saremi na mashahidi waandishi wa habari katika kipindi chote cha Mapinduzi ya Kiislamu, na tunaziombea taasisi zote mafanikio salama na sahihi.
Akaendelea kubainisha: Wakoloni ambao katika karne ya hivi karibuni walijitosa kwenye uporaji wa mali, walikuja pamoja na majeshi yao, lakini pia walikuwa na jeshi lingine lenye umbo tata – ambalo ni vyombo vya habari vya kikoloni na vya kibepari. Kwa karne kadhaa, vyombo vya habari katika nchi za Magharibi vilikuwa mateka wa ubeberu na ukoloni, habari zilipotoshwa, harakati batili ziliimarishwa, mataifa yakapigwa sindano ya ulevi wa fikra, na njia za ukoloni na uporaji zikalainishwa, hii ni "ngoctopus" ya vyombo vya habari vya Kimagharibi ambayo iliweka mataifa chini ya utumwa, huu ndio mfano wa vyombo vya habari vya batili na vya kishetani.
Mapinduzi tukufu ya taifa kubwa la Iran yalijenga mfumo mpya wa habari
Mkurugenzi wa taasisi za kielimu za Hawza nchini Iran alibainisha kuwa: Mapinduzi Tukufu ya taifa kubwa la Iran yaliweka msingi wa mfumo mpya wa habari, na yakavunja mahesabu ya kikoloni ya vyombo vya habari vya Kimagharibi, wawakilishi wa habari wa kweli na waaminifu waliubadilisha mwelekeo wa vyombo vya habari vya Kimagharibi katika mhimili wa muqawama, ulimwengu wa Kiislamu, na Iran. Mashahidi kama Saremi, Sahar Emami na waandishi wa habari waaminifu, wachamungu na mashujaa walikuwa katika huduma ya mataifa, na wakaonesha njia ya ukombozi, hiki ndicho chombo sahihi cha habari.
Akasema: Vyombo vya habari vinapaswa kuwa katika huduma ya watu, vipunguze mateso na maumivu yao, na viandae mazingira ya kukua na kupata ukamilifu, kamwe visiwe chanzo cha kutikisa nyoyo, kudhoofisha jamii na misingi ya maadili, thamani kubwa ya kalamu na chombo cha habari ni kuwa katika huduma ya mwanadamu, ukamilifu wake na ukombozi wake.
Shukrani kwa Vyombo vyote vya Habari
Imamu wa Ijumaa wa Qom aliendelea kusena: Tunazishukuru taasisi zote za habari zilizo salama na zenye uaminifu. Katika vita vya habari, chombo cha habari ndicho kinachopaswa kufikisha simulizi sahihi kwa vijana na jamii, na kuonesha njia ya ukuaji na ukamilifu, chombo cha habari kilicho fanikiwa ni kile kinachoweza kuwasilisha ukosoaji na upinzani kwa njia sahihi, taasisi zote zinapaswa kushirikiana na chombo sahihi cha habari, Idara za uhusiano wa umma, vyombo vya habari huru na vya kujitegemea vinapaswa kuwa zana za kukuza na kuinua watu.
Mkurugenzi wa Hawza aliongeza kusema: Mwezi wa Mordad unakumbusha matukio mawili makubwa ya kihistoria – harakati ya Mashruta na harakati ya mafuta, katika kurasa hizi mbili za historia, kuna mafunzo muhimu yaliyofichika. Imam Khomeini (ra) aliitazama historia hii na kuweka msingi na usanifu wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Sababu Nne za Kufa kwa Harakati ya Mashruta
Katika sehemu nyingine ya hotuba yake alisema: Harakati ya Mashruta ilizaliwa katika enzi ya Qajar, wakati dunia ilikuwa inaingia katika mabadiliko ya kielimu na kiteknolojia, harakati hii ilitokana na mwamko wa watu, kilio dhidi ya mfumo wa kifalme na uongozi wa wanavyuoni na watu wakubwa wa dini, na ilikuwa na malengo mazuri.
Harakati hii iliungwa mkono na wanavyuoni wa Najaf, marjaa wakubwa, na viongozi mashuhuri, na ilichukua hatua kubwa dhidi ya dhulma ya kifalme kwa ajili ya uhuru na kujitegemea kwa nchi, lakini harakati hii kubwa ya kitaifa ilikumbwa na matatizo kadhaa.
Sababu ya Kwanza: Ukosefu wa Nadharia Kamili ya Mashruta
Khatibu wa Swala ya Ijumaa ya Qom alihusisha matatizo haya na sababu mbalimbali, na akasema: Moja ya sababu ni ukosefu wa nadharia kamili kuhusu Mashruta, harakati ya Mashruta haikuwa na msingi mpana wa kifikra kuhusu uhuru na kujitegemea kwa nchi, na kwa hiyo ikakumbwa na matatizo.
Sababu ya Pili: Muda wa Wavamizi wa Kigeni
Alitaja uingiliaji wa wageni kuwa sababu ya pili na akasisitiza kuwa: Uvamizi wa wageni kama Uingereza na nguvu za kishetani za wakati huo uliivuruga harakati ya Mashruta na kuiangamiza misingi yake sahihi.
Sababu ya Tatu na ya Nne: Usaliti wa Walioathirika na Magharibi na Kutojitambua kwa Wanaohusika na Udhaifu wa Basira
Ayatollah A'rafi alitaja pia sababu ya tatu na ya nne akasema: Usaliti wa watu waliovutwa na fikra za Magharibi, ambao hawakuelewa kuwa uhuru na kujitegemea nchini Iran umefungamana na Uislamu, pamoja na kutojitambua kwa waliohusika katika Mashruta na udhaifu wa basira yao, ni sababu nyingine muhimu.
Mkurugenzi wa Hawza aliongeza: Sababu hizi zote ziliungana na kusababisha harakati ambayo ingeweza kuwa chanzo cha mwamko na ukombozi wa Iran kuwa vurugu, mgawanyiko, mfarakano, na kuachana na misingi ya dini, jambo ambalo matokeo yake ilikuwa ni kuibuka kwa utawala wa Pahlavi, ni jambo la kusikitisha kwamba kutoka katika harakati ya kudai uhuru, alizaliwa mfalme muovu kama Reza Khan.
Akaendelea kusema: Familia ya Pahlavi iliweka msingi wa utegemezi kwa Magharibi, wakati ambapo utegemezi kama huo haujawahi kutokea katika historia ya Iran. Zamani, tulikuwa na wafalme dhalimu, madikteta na wakatili, lakini utegemezi wa wazi na wa dhahiri kwa Marekani na Uingereza ulikuwa msiba mkubwa ulioanzishwa kwa mara ya kwanza na ukoo wa Pahlavi.
Imamu wa Ijumaa wa Qom aliongeza kuwa: Iran ya Kiislamu katika vita vya siku kumi na mbili ilionyesha kwamba mwamko wa wananchi, uongozi wa kipekee na madhubuti, elimu na maarifa ya majeshi ya ulinzi, na mshikamano wa taifa vinaweza kuzivuruga njama zote, na hii ilikuwa ni fahari kubwa ambayo nyinyi mliiweka.
Mafunzo yanayo patikana katika vita ya siku 12
Somo la kwanza: Kuutegemea uwezo wa ndani
Akaeleza kwamba: Vita hivi vikubwa vya kihistoria na kiutamaduni vilitufundisha somo la kujiamini na kutegemea nguvu zetu za ndani. Kujiamini kitaifa na kutegemea uwezo wa ndani ni msingi wa maendeleo. Tunakubali mawasiliano na uhusiano na dunia kwa masharti yake, lakini msingi wetu imara ni sisi wenyewe, na kujiamini ndani ndiko kunakoleta wokovu.
Somo la pili: Umuhimu wa kumfahamu zaidi adui na hila zake
Mkurugenzi wa Hawza nchini Irani aliongeza kuwa: Kumfahamu adui kwa kina na kutomwogopa lilikuwa ni somo la pili, lazima tumtambue adui, hata katika mazungumzo naye kuna udanganyifu. Ujasiri wa kusimama dhidi ya adui, kumfahamu kwa undani, na kuwa na basira (uelewa wa kina) ni mambo yaliyokuwa na athari katika vita hivi, leo pia hatupaswi kuogopa vita, taifa letu ni watu wa vita na mapambano magumu, na kinachopaswa kuogopwa ni hila na njama zilizo ngumu zaidi.
Somo la tatu: Mantiki ya dunia ni nguvu na uwezo wa kushawishi
Akaongeza kuwa: Vita vya kulazimishwa vya siku 12 vilionyesha kuwa mantiki inayoongoza dunia ni ya nguvu, na uwezo (wa kushawishi na kushinda) ni lazima, Hata kama utakuwa katika haki kiasi gani, hakuna atakayekusikiliza, tunapaswa kuunda na kuimarisha aina nane za uwezo: uwezo wa kielimu na kimaarifa na kifikra na kidhana, uwezo wa kiroho, kimaadili na kitamaduni, uwezo wa kisayansi na kiteknolojia, uwezo wa kijamii na mshikamano wa kitaifa, uwezo wa kisiasa kwa msingi wa demokrasia ya kidini na uongozi wa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi, uwezo wa kiuchumi, kijeshi na kiusalama, na uwezo wa kimataifa.
Somo la nne: Tusidanganyike kwa ahadi za adui
Khatibu wa Ijumaa wa Qom kwa kusisitiza kuwa hatupaswi kudanganyika na adui, alisema: pipi zilizotiwa sumu, glavu za hariri na matawi ya mizeituni ya uongo kutoka kwa adui si suluhisho la matatizo wala si njia ya kutatua mambo, nchi za Kiislamu duniani nazo lazima zijue hili.
Akaongeza kues: Leo serikali ya Lebanon ni mkusanyiko wa mataifa ya Kiislamu, msije mkadanganyika kwa ahadi za pipi zilizotiwa sumu za Marekani na kuwanyang’anya silaha Hizbullah, Hizbullah ndiyo iliyowakomboa, kama mtanyang’anywa upanga huu, mtakuwa kama Syria na Libya, serikali na bunge la Lebanon leo ni wawakilishi wa umma wote wa Kiislamu, Msidanganyike kwa ahadi za uongo za Trump na nguvu za Magharibi, tegemeeni misingi yenu, na wekeni imani yenu kwa silaha ya mapambano.
Imamu wa Ijumaa wa Qom alisema: Kuondoa silaha na mpango wa mataifa mawili kwa ajili ya Palestina ni hila ya kuipiga umma wa Kiislamu. Ahadi zote za adui ni uongo, adui aliingia vitani katikati ya mazungumzo, tunatarajia dunia ya Kiislamu iwe macho na isidanganyike, bali kwa mshikamano, maelewano na mshikamano wa kweli na uwezo, ipite katika njia ya heshima na uhuru wake.
Maoni yako