Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza, Mtukufu Ayatollah Khamenei amejibu istiftaa kuhusiana na “kuweka picha na video binafsi kwenye wasifu”, jibu ambalo linawasilishwa kwa wasomaji na wapenda mada hizi kama ifuatavyo.
Swali:
Je, Mtu kuweka picha na video zake katika mitandao ya kijamii (wasifu na kadhalika) kuna tatizo? (Kwa kuwa mimi ninaona kwamba watu wengi wa dini na wa mapinduzi hujiepusha na kuweka picha na video zao katika mitandao ya kijamii.)
Jawabu:
Kwa upande wa wanaume, kiasili hakuna kizuizi; lakini kwa upande wa wanawake, iwapo watakuwa bila hijabu ya kisheria, kwa mujibu wa tahadhari ya lazima (ihtiyāt wājib), haijuzu.
Maoni yako