Kwa mujibu wa Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, Hizbullah iliandaa hafla ya kuwakumbuka makamanda mashahidi (Sayyid Abbas Mousawi, Sheikh Ragheb Harb na Hajj Imad Mughniyeh) katika Raudha ya Sheikh al-Shuhadaa katika mji wa Jabshit; hafla iliyohudhuriwa na Sheikh Abdulkarim Ubayd, idadi ya wanaharakati, familia za mashahidi na wakazi wa eneo hilo.
Katika hafla hiyo, Sheikh Ubayd alisisitiza kuwa; njia na mwenendo wa makamanda mashahidi utaendelea kuwa dira ya kuongoza safari. Aliongeza kuwa, kujitoa mhanga walikokutoa hakukuwa kituo cha mpito tu, bali kuliweka msingi wa hatua mpya yenye jina la uthabiti na heshima.
Alieleza wazi kwamba uaminifu wa kweli ni kuendelea kutembea katika njia hiyo hiyo na kusimama imara juu ya chaguo la muqawama mbele ya changamoto zote; kwa kuwa harakati iliyoanza kwa damu ya makamanda haitasimama kamwe maadamu ndani ya umma bado inapiga mdundo wa uhuru na irada thabiti.
Katika hafla hiyo, makaburi ya mashahidi huko Jabshit yalishuhudia ushiriki mpana wa wajumbe kutoka sekta za kitaaluma, kielimu, kiafya, kitamaduni na kijamii. Aidha, makundi ya majeruhi wa muqawama wa Kiislamu, Kamati ya Usaidizi ya Muqawama wa Kiislamu, Taasisi ya Shahidi, wahudumu wa uokozi wa ulinzi wa kiraia chini ya Kamati ya Afya ya Kiislamu, Shirika la Skauti la Imam Mahdi (Mwenyezi Mungu aharakishe kudhihiri kwake), Jumuiya ya Misaada na Mkusanyiko wa Walimu walihudhuria hafla hiyo.
Maoni yako