Jumapili 22 Februari 2026 - 15:40
Chapisho la Uongozi wa wanazuoni ni ramani ya njia ya Hawza inayolingana na Mapinduzi ya Kiislamu

Hawza/ Chapisho la Uongozi wa wanazuoni ni ramani ya njia ya Hawza inayolingana na Mapinduzi ya Kiislamu; Hawza ambayo haiangukii katika ukakasi na mgando wa fikra (tahajjur), wala haitegwi na michezo ya kisiasa ya makundi na itikadi za kiliberali.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza,  Kituo cha Usimamizi wa Hawza za Kielimu kimetoa bayana kutokana na mnasaba wa kumbukumbu ya miaka thelathini na saba tangu kutolewa kwa chapisho la Uongozi wa uwanazuoni.

Katika bayana hiyo imeelezwa kuwa:

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu

“Salamu juu ya watengenezaji wa hamasa wa milele wa uwanazuoni ambao risala yao ya kielimu na ya kiutendaji waliiandika kwa pumzi ya shahada na wino wa damu, na juu ya mimbari ya uongofu na mawaidha na kuwahutubia watu, kutokana na mshumaa wa uhai wao walitengeneza lulu ya mwanga wa usiku. Fahari na pongezi kwa mashahidi wa Hawza na wanazuoni ambao katika wakati wa mapambano walikata kamba za mafungamano ya darsa, mijadala na madrasa, wakaondoa kitanzi cha matamanio ya dunia kutoka katika mguu wa haki ya elimu, na kwa wepesi wakaenda katika ugeni wa viumbe wa juu na katika mkusanyiko wa malaika wakaimba shairi la uwepo.” (Hati ya Uongozi wa wanazuoni)

Majira ya kuchipua ya thelathini na saba yamepita tangu mwangwi wa sauti ile ya kengele iliyozoeleka; wito mtukufu wa Marji' ambaye mwangwi wake ulienea hadi upeo wa milele na kuziita Hawza za Kielimu kwa tafakuri mpya kwenye historia yote. Hati ya Uongozi wa Uwanazuoni ni mkataba wa milele wa Mwanzilishi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Imam Khomeini (r.a), ambao kwa hakika ni wasia wa kisiasa–kiungu wa kiongozi huyo wa Kiungu kwa vizazi mfululizo vya wanahawza hadi kufikia malengo ya juu ya Mapinduzi ya Kiislamu.

Kituo cha Usimamizi wa Hawza za Kielimu, huku kikihuisha kumbukumbu ya mashahidi wanazuonk ambao Imam Marehemu aliita damu yao safi “iliyopaka wekundu upeo wa fiqhi”, kinasisitiza mihimili mikuu ya hati hii ya Kiungu ambayo ni mwongozo wa milele wa Hawza, na kinaweka maonyo yake ya kuelimisha mbele ya macho yake, na kwa umakini kinafuatilia hatari ya kupenya fikra potofu kwa jina la dini; kama ambavyo katika historia tukufu ya Ushia, “ngome imara zaidi ya Uislamu dhidi ya mashambulizi, upotovu na mienendo ya kupotoka” imekuwa ni wanazuoni.

Chapisho la Uongozi wa wanazuoni ni ramani ya njia ya Hawza inayolingana na Mapinduzi ya Kiislamu; Hawza ambayo haiangukii katika fikra mgando, wala haishikwi na mitego ya michezo ya kisiasa ya makundi na kiliberali. Hawza ambayo Imam Khomeini (r.a) aliihusu kwa kusema: “Katika kueneza wanazuoni na fiqhi, hakukuwa na nguvu ya mkuki wala mtaji wa wapenda pesa na matajiri; bali ni sanaa, uaminifu na kujitolea kwao wenyewe ndiko kulikowafanya watu wawachague.”

Kituo cha Usimamizi wa Hawza za Kielimu, huku kikihuisha ahadi kwa malengo ya Imam Marehemu na Kiongozi Mwenye Hekima wa Mapinduzi, Mtukufu Ayatullah al-Udhma Khamenei (Mwenyezi Mungu amlinde), kinajiona kuwa ni wajibu wake kufundisha na kufafanua hati hii katika ngazi mbalimbali za Hawza, na kuitambulisha kizazi cha vijana wa Hawza undani wa wasia huu wa Kiungu, na kuendeleza njia ya mashahidi ambao “walikata kamba za mafungamano ya darsa, mijadala na madrasa, wakaondoa kitanzi cha matamanio ya dunia kutoka katika mguu wa haki ya elimu, na kwa wepesi wakaenda katika ugeni wa viumbe wa juu.”

Tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu atujalie kuwa miongoni mwa watumishi wa kweli wa Qur’ani na Ahlul-Bayt, na askari wa hakika wa Mtukufu Waliyul-‘Asr (a.f).

Kituo cha Usimamizi wa Hawza za Kielimu.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha