Jumanne 16 Desemba 2025 - 00:30
Radi Amali ya Kamati ya Uongozi wa Michezo ya Hawza Nchini Iran, Kuhusu “Mechi ya Kifahari ya Mashoga”

Hawza/ Kufuatia kuitwa kwa mchezo wa timu ya taifa ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Jamhuri ya Kiarabu ya Misri kwa jina la “Mechi ya Fahari” (Pride Match) na FIFA pamoja na Kamati ya Maandalizi ya Mashindano ya Kombe la Dunia la mpira wa miguu 2026, yatakayofanyika katika mji wa Seattle, Marekani, kwa lengo la kuunga mkono ushoga, Kamati ya Uongozi wa Michezo ya Hawza imetoa tamko.

Kwa mujibu wa ripoti ya mwandishi wa Shirika la Habari la Hawza, kufuatia kuitwa kwa mchezo kati ya timu ya taifa ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Jamhuri ya Kiarabu ya Misri kwa jina la “Mechi ya Fahari” (Pride Match) kwa ajili ya kuunga mkono ushoga, Kamati ya Uongozi wa Michezo ya Hawza imetoa tamko, ambalo maandishi yake ni kama ifuatavyo:

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye kurehemu

وَلَا تَقْرَبُوا الْفَوَاحِشَ مَا ظَهَرَ مِنْهَا وَمَا بَطَنَ
“Wala msikaribie machafu, yaliyo wazi na yaliyo fichika.”
(Sura Al-An‘ām, Aya ya 151)

Uamuzi wa FIFA na Kamati ya Maandalizi ya Mashindano ya Kombe la Dunia la mpira wa miguu 2026 katika mji wa Seattle, Marekani, wa kuuita mchezo wa timu ua taifa ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Jamhuri ya Kiarabu ya Misri kwa jina la “Mechi ya Fahari” (Pride Match) kwa lengo la kuunga mkono ushoga, kwa upande mmoja unaleta mshangao, na kwa upande mwingine unasababisha masikitiko makubwa.

Kamati ya Uongozi wa Michezo ya Hawza inauona uamuzi huu kuwa ni matusi ya wazi kwa itikadi za kidini za mamia ya mamilioni ya Waislamu wa Iran na Misri, na mabilioni ya Waislamu kote duniani, pamoja na wafuasi wa dini zote za mbinguni.

Uislamu unatangaza wazi kwamba; ushoga ni kitendo kilichoharamishwa, kichukizacho na miongoni mwa madhambi makubwa. Kwa hiyo, kwa kuzingatia mafundisho ya Mwenyezi Mungu na maadili ya kibinadamu, tunawaomba wahusika husika yafuatayo:

1- Wizara ya Michezo na Vijana na Shirikisho la Mpira wa Miguu la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran lazima:

1- Kuharakisha kuwasilisha pingamizi lao rasmi na la wazi kupitia njia za kidiplomasia na kisheria za kimataifa kwa FIFA, na kudai kufutwa mara moja kwa jina hili na programu zozote zinazohusiana nalo.
2- Endapo FIFA haitazingatia, waweke kwa umakini changanuzi zote zinazowezekana katika ajenda, ikiwemo kukataa kushiriki katika mchezo huu chini ya jina hili.

2- Uongozi wa Kidini wa Ulimwengu wa Kiislamu (hasa Maraji' Wakuu wa Taqlidi wa Hawza ya Elimu ya Dini ya Qum na Al-Azhar Tukufu)
1- Kwa kutoa tamko thabiti, wautangazie tena ulimwengu msimamo wa kidini wa Uislamu kuhusu kuharamishwa kabisa kwa ushoga, na kuiomba FIFA, kwa kuheshimu dini, isitumie michezo kama chombo cha kueneza maadili potofu yanayokinzana na Sharia.
2- Waalike taasisi zote za Kiislamu za kimataifa kushiriki katika pingamizi hili la pamoja.

3- Mashirika ya Kiislamu na ya Kidini ya Kimataifa

1- Ipinge vikali hatua hii ya FIFA;
2- Iwatake FIFA katika sera zake izingatie heshima kwa dini na kwa maadili ya kibinadamu ya mataifa mbalimbali.

Tunaamini kwa dhati kwamba; michezo inapaswa kuwa uwanja wa urafiki, heshima kwa pande zote kati ya mataifa na kueneza amani, si uwanja wa kulazimisha mitindo ya maisha na itikadi ambazo zinakinzana kwa kina na imani za mabilioni ya watu.

Kwa hiyo, katika kuthibitisha madai ya kutokuwa na upendeleo ya FIFA na heshima kwa maadili ya kitamaduni, kibinadamu na kidini, tunadai kuombwa radhi rasmi na FIFA pamoja na Kamati ya Maandalizi ya Mashindano kwa wafuasi wa dini za mbinguni, Waislamu dunianj hususan mataifa ya Iran na Misri, kufutwa mara moja na kwa ujumla jina hili na programu au nembo yoyote inayohusiana nalo kwa mchezo huu, na kutangazwa kwa dhamana zinazohitajika kutoka kwa FIFA kwamba vitendo kama hivi vya kudhalilisha, vinavyokosa heshima kwa heshima za kidini za mataifa, havitarudiwa tena.

Kamati ya Uongozi wa Michezo ya Hawza

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha