Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza, tutakuwa na “Aya zinazohusiana Maisha” ambazo ni mfululizo wa aya za Qur’ani Tukufu pamoja na tafsiri fupi na inayotumika katika maisha, zinazotufundisha namna ya kuishi maisha bora na kufikia mafanikio. Tutaongeza nuru katika siku za Ramadhani kwa neno la Mwenyezi Mungu kupitia aya hizi.
Hujjatul-Islam na Muslimin Hadi Hussein Khani
Bismillah Rahman Rahim; Aya ya 90 Surah An-Nahl:
«إِنَّ اللَّهَ یَأْمُرُ بِالْعَدْلِ وَالْإِحْسَانِ وَإِیتَاءِ ذِی الْقُرْبَیٰ وَیَنْهَیٰ عَنِ الْفَحْشَاءِ وَالْمُنْکَرِ وَالْبَغْیِ یَعِظُکُمْ لَعَلَّکُمْ تَذَکَّرُونَ»
Mwenyezi Mungu anatufundisha katika aya hii kuhusu kufanya uadilifu, wema, na kuwasaidia ndugu, na pia anatufundisha kuepuka maovu, maasi na dhuluma. Mwenyezi Mungu anawafundisha ili mpate kukumbuka.
Aya hii ina maelezo muhimu:
1. Umuhimu wa kuamrusha mema na kukataza Munkar: Ambapo wakwanza kuamrisha mema na kukataza maovu ni Mwenyezi Mungu mwenyewe:
«إِنَّ اللَّهَ یَأْمُرُ بِالْعَدْلِ وَالْإِحْسَانِ...».
2. Wema kwa familia: Katika kutendea wema, ndugu ndio wanaopewa kipaumbele. Mwenyezi Mungu anasema: «إِنَّ اللَّهَ یَأْمُرُ بِالْعَدْلِ وَالْإِحْسَانِ وَإِیتَاءِ ذِی الْقُرْبَیٰ», yaani, mtoe msaada kwa familia zenu.
3. Kuepuka maovu: Anaonya kuepuka maovu, maasi na dhuluma. Katika hili, «fahsha» inahusu madhambi yaliyo dhahiri na mabaya, ambayo Mwenyezi Mungu anakataza kwanza. Kisha anakataza maovu mengine na dhuluma kwa watu wengine.
4. Mafundisho na maonyo: Mwenyezi Mungu anatufundisha kupitia mafundisho (muwajih) ambayo huathiri moyo wa binadamu, tofauti na amri kavu na kali. Huu mtindo wa mafundisho unapanua nafasi ya kujua ukweli na kufuata njia ya haki.
5. Matokeo ya mafundisho: Katika mwisho wa aya, Mwenyezi Mungu anasema: «لَعَلَّكُمْ تَذَكَّــرُونَ», maana yake ni kwamba huenda mtakumbuka. Hii inadhihirisha kwamba, matokeo ya kuamrisha mema na kukataza munkar sio daima kama tunavyotaka, bali huenda mtu akakumbuka na kubadilika.
Hii ni kwa sababu, mema na mabaya vimejikita kwenye fitra ya binadamu, na tunapokumbusha, tunawasaidia kukumbuka hayo.
Maoni yako