Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, taarifa zinaonyesha kuwa wahamiaji haramu wa Kizayuni wanajihusisha na utaifishaji wa kutisha wa mali za makanisa ya Orthodox, hasa katika eneo la Ukingo wa Magharibi.
Miongoni mwa makanisa yaliyotaifishwa, ni Kanisa la kihistoria la Mtakatifu Gerasimos lililoko karibu na mji wa Yeriko, kwa mujibu wa ushahidi, mvutano katika eneo la Yeriko umeongezeka sana katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, na kuna uwezekano wa mali nyingine pia kutwaliwa kinyume cha sheria na wahamiaji haramu wa Kizayuni.
Katika muktadha huo huo, kikao cha dharura cha uchambuzi na ufuatiliaji kimefanyika mjini Athene ili kuchunguza na kutathmini hali ya ugawaji haramu wa ardhi za makanisa huko Baitul Muqaddas.
Chanzo: Shirika la Habari la Anadolu
Maoni yako