Alhamisi 7 Agosti 2025 - 22:33
Njama ya Pamoja Iraq na Lebanon; Marekani Yataka Muqawama Usalie Bila Silaha

Hawza/ Mjumbe mmoja wa Baraza la Kisiasa la Harakati ya Nujabaa ameonya kuwa Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel (kwa kushirikiana na serikali ya Lebanon) wanaendeleza mipango ya kudhoofisha mshikamano wa ndani na kuzivua silaha harakati za muqawama nchini Lebanon na Iraq.

Kwa mujibu wa idara ya kimataifa ya  Shirika la Habari la Hawza, Dkt. "Firas al-Yasir", mjumbe wa Baraza la Kisiasa la Harakati ya Nujabaa, amesema: Kama ambavyo Marekani na Israel (kwa kushirikiana na serikali ya Lebanon) wametekeleza siasa za kuchochea mfarakano na kutoa vitisho ili kudhoofisha mshikamano wa ndani na kuivua silaha Hizbullah, mpango kama huo pia unatekelezwa Iraq, kwa lengo la kuishambulia Al-Hashd al-Shaabi, kuzuia kutambuliwa kwake kisheria, na kuchochea mifarakano baina ya makundi ya Kishia na serikali.

Ameongeza kuwa: Matokeo ya njama hii yatakuwa ni hali ya kukosekana kwa utulivu na machafuko katika eneo hili, kwa sasa, serikali ya Iraq inakabiliwa na mtihani mpya, na haipaswi kusimama dhidi ya matakwa ya wananchi.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha