Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, mwaka 1370 H.Sh., Hussein Kamel alivamia Haram ya Imam Hussein (as) kwa amri ya Saddam Hussein na kuishambulia kuba tukufu, lakini hatima yake iliandikwa kwa usaliti na kuuawa na familia yake mwenyewe.
Mwisho wa Kujigamba dhidi ya Imam Hussein (as)!
Katika harakati ya Kishia ya Karbala mwaka 1370 H.Sh., Saddam Hussein alimpa mkwe wake, Hussein Kamel, amri huku akisema: "Vamieni Haram ya Hussein (as) na muwakatakata vipande watu wote waliopo humo!"
Hussein Kamel alisimama mlangoni mwa Karbala, akaanza kujigamba kwa majivuno na ujasiri, akasema: "Mimi ni Hussein na wewe pia ni Hussein. Tuone ni nani atakayemuangamiza mwenzake kwanza!"
Kisha akaelekeza risasi za kifaru moja kwa moja kwenye kuba ya Harem ya Imam Hussein (as).
Chini ya miaka minne baadaye, Hussein Kamel alijitenga na Saddam, na akaikimbia Iraq pamoja na ndugu yake Saddam Kamel na wake zao – Raghd na Rana (binti za Saddam) – na wakakimbilia Jordan ili kutafuta hifadhi ya kisiasa Marekani. Wamarekani walimpa jina la "Sanduku la Siri za Saddam."
Baada ya Shirika la CIA kumchukua na kuchukua taarifa zote kutoka kwake, walimwambia: "Kwa kuwa wewe ulikuwa mkuu wa viwanda vya kemikali vya Iraq na umetenda jinai nyingi, hatuwezi kukupa hifadhi ya kisiasa."
Aliomba kwa unyenyekevu sana, lakini hakufaulu, Serikali ya Jordan pia ilimwambia kuwa lazima aondoke haraka kutoka nchini humo. Saddam Hussein alimtumia barua ya msamaha na kumwambia kuwa amemsamehe na anaweza kurudi Iraq.
Hussein Kamel, licha ya kumfahamu vyema Saddam na hulka yake ya kinyama, alilazimika kurejea Iraq.
Uday, mwana wa Saddam, alikwenda kwenye nyumba aliyokuwa akiishi Hussein Kamel, na baada ya kumpiga sana, aliwalazimisha ndugu wawili hao kutia saini hati za talaka kwa wake zao, Raghd na Rana.
Saddam, kisha akawaita baba na ndugu wa Hussein Kamel kwenye kasri lake, akawapa silaha na kuwaambia: "Ninyi wenyewe mnapaswa kulifuta doa hili la aibu kutoka kwenye ukoo wenu."
Usiku wa Ijumaa, tarehe 1374/12/4 H.Sh., familia ya Kamel ilizingira nyumba hiyo na kuwaua ndugu hao wawili.
Hatimaye, mtu aliyedhamiria kuiangamiza Haram ya Aba Abdillah (as) aliangamizwa kwa mikono ya familia yake mwenyewe, lakini Haram ya Imam Hussein (as) leo hii, hasa katika msimu wa Arbaeen, inawakaribisha kwa fahari mamilioni ya waumini kutoka kila pembe ya dunia.
Maoni yako