Jumatatu 28 Julai 2025 - 07:15
Mwanachama wa Jumuiya ya Walimu wa Hawza ya Qom: Ukimya unaofanywa na nchi za kiislamu mbele ya mauaji ya kimbari ya watu wa Ghaza ni aibu

Hawza/ Ayatullah Tabasi amesema: Hii leo ukimya mbele ya jinai zinazofanywa na utawala wa Kizayuni muuaji wa watoto ni usaliti, ukimya unaofanywa na baadhi ya nchi za Kiislamu mbele ya mauaji ya kimbari ya Waislamu wanyonge wa Ghaza kweli ni aibu.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Najmuddin Muruji Tabasi, katika hafla ya usiku wa pili wa mwezi wa Safar iliyofanyika, huku ikuhudhuriwa na wanazuoni pamoja na waumini wa Qom katika nyumba ya Ayatullah Shah Abadi (r.a), akiirejea aya ya 159 ya Surah Baqarah:

«إِنَّ الَّذِینَ یَکْتُمُونَ مَا أَنْزَلْنَا مِنَ الْبَیِّنَاتِ وَالْهُدَیٰ مِنْ بَعْدِ مَا بَیَّنَّاهُ لِلنَّاسِ فِی الْکِتَابِ ۙ أُولَٰئِکَ یَلْعَنُهُمُ اللَّهُ وَیَلْعَنُهُمُ اللَّاعِنُونَ»

Hakika wale wanao ficha tuliyo yateremsha -- nazo ni hoja zilizo wazi na uwongofu baada ya Sisi kuzibainisha kwa watu Kitabuni -- hao anawalaani Mwenyezi Mungu, na wanawalaani kila wenye kulaani.
(Baqara: 159)

Amesema: Aya hii inawaashiria wazi wale wanaojua ukweli lakini wanakataa kuusema.

Amesisitiza kwa kurejelea mitazamo ya wafasiri kuwa: Baadhi ya watu wa elimu wameona mfano wa aya hii kuwa ni kwa watu wa Kitabu kama Mayahudi na Wakristo, miongoni mwao ni Ka‘b bin Ashraf na Asad bin Suriya ambao katika zama za Mtume Mtukufu (s.a.w\.w) wakiwa wanajua ukweli wa Uislamu waliuficha na wakapata ghadhabu ya Mwenyezi Mungu.

Mtume (s.a.w\.w) na Ahlul-Bayt (a.s) katika Kukabiliana na Kufichwa kwa Ukweli

Mjumbe huyu wa Jumuiya ya Walimu wa Hawza ya Qom akielezea sira ya Mtume (s.a.w\.w) amesema: Mtume Mtukufu (s.a.w\.w) katika kukabiliana na fitina wakati mwengine aliwateua watu maalumu ili iwapo patakuwepo haja wachukue hatua kali, mfano ni kuuawa kwa Ka‘b bin Ashraf kwa amri ya moja kwa moja kutoka kwa Mtume (s.a.w\.w).

Ayatullah Tabasi ameendelea kusema kuwa: Maimamu Maasum (a.s) pia katika nyakati nyeti walitumia njia zinazolingana na mazingira ya zama zao ili kufichua ukweli, Imam Hadi (a.s) ni mfano wa utekelezaji wa sira hii katika zama zake.

Wengine Wakificha Ukweli kwa Kuitumia Dini vibaya

Ameongeza kwa kusema: Leo hii baadhi ya watu kwa kuitumia vibaya dini wanaficha ukweli kwa watu, kama watu wangejua yaliyopita na yanayoendelea, wasingewafuata baadhi ya watu, wale wanaoingia katika medani nyeti kama uchaguzi wanapaswa kuwa na sifa za kweli, sio kuficha ukweli na kudai utiifu wa milele.

Mwalimu huyu wa Hawza amekosoa baadhi ya fikra za kiubinafsi akisema: Baadhi wanajiona kuwa wao ndio kipimo cha haki na wanaamini yeyote anayepinga maamuzi yao anastahili kifo, fikra hii ni hatari, si ya kidini wala ya kiakili.

Onyo Kuhusu Kupotosha Historia na Kunyakua Nafasi za Watu

Ayatullah Tabasi katika sehemu nyingine amesema kuwa: Baadhi kwa kupotosha historia na kuficha majina ya wafuasi wa kweli wa Ahlul-Bayt (a.s) wanajaribu kuondosha sura za watu, katika baadhi ya vyanzo vimeorodheshwa majina ya watu 170 miongoni mwa Masahaba na Tabi‘in waliokuwa wafuasi wa kweli wa Ahlul-Bayt (a.s).

Mjumbe huyu wa Jumuiya ya Walimu wa Hawza ya Qom pia ameashiria kuandikwa kwa usahihi kwa majina na ripoti katika vitabu vya kihistoria na kuongeza kuwa: Katika vyanzo vya Kishia, majina ya watoto na wafuasi wa Imam Ali (a.s), Imam Musa bin Ja‘far (a.s) na Maimamu wengine yamekuja waziwazi, lakini baadhi wanajaribu kudhoofisha nyaraka hizi.

Leo Ukimya Mbele ya Jinai za Utawala wa Kizayuni Ni Usaliti

Amesisitiza umuhimu wa ujasiri katika kusema ukweli akasema: Baadhi ya watu hata katika kusoma dua na salamu kwa Ahlul-Bayt (a.s) wanapata shaka na hofu, ilhali mbele ya dhulma na ufisadi, inapaswa kuwa mwangaza na kusema ukweli.

Mtafiti huyu wa Hawza amesema: Leo ukimya mbele ya jinai za utawala wa Kizayuni muuaji wa watoto ni usaliti. Ukimya wa baadhi ya nchi za Kiislamu mbele ya mauaji ya kimbari ya Waislamu wanyonge wa Ghaza kweli ni aibu.

Hitimisho la utawala bandia wa Kizayuni lipo karibu 

Mwisho wa risala yake amesema kuwa: "Inshaallah" hatamu ya utawala bandia wa Kizayuni iko karibu, kabla ya kudhihiri Imam wa Zama (a.f), utawala wa Israel na serikali ya Kiyahudi vitahilikishwa, na katika zama za kudhihiri kwa Imam Mahdi (a.f) hakutakuwepo na dola iitwayo Uyahudi au Israel.

Mwisho wa ujumbe

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha