Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, kufuatia mauaji ya kizazi yanayofanywa na utawala wa kizayuni mavamizi katika Ukanda wa Ghaza, Jumuiya ya Walimu wa Hawza ya Qom imekutoa barua ya wazi, na kuwataarifu maulamaa na wasomi wa ulimwengu wa Kiislamu kutekeleza jukumu lao la kibinadamu na Kiislamu kwa watu wa Ghaza.
Matini ya barua hiyo ni kama ifuatavyo:
Bismillāhi ar-Raḥmāni ar-Raḥīm
Al-ḥamdu lillāhi Rabbil-ʿālamīn wa ṣallallāhu ʿalā nabiyyinā Muḥammad Rasūlillāh wa ʿalā ālihi al-ṭāhirīn wa ṣaḥbihi al-muntajabīn
قال الله تعالی فی کتابه الکریم:
«وَ ما لَکُمْ لا تُقاتِلُونَ فی سَبیلِ اللَّهِ وَالْمُسْتَضْعَفینَ مِنَ الرِّجالِ وَالنِّساءِ وَالْوِلْدانِ الَّذینَ یَقُولُونَ رَبَّنا أَخْرِجْنا مِنْ هذِهِ الْقَرْیَةِ الظَّالِمِ أَهْلُها وَ اجْعَلْ لَنا مِنْ لَدُنْکَ وَلِیًّا وَاجْعَلْ لَنا مِنْ لَدُنْکَ نَصیرا»(Na kwa nini msipigane katika njia ya Mwenyezi Mungu na kwa ajili ya wanaume wanyonge, wanawake na watoto, ambao husema: Mola wetu! Toa kutoka katika kijiji hiki ambacho watu wake ni madhalimu, na tujaalie kutoka kwako mlinzi, na tujaalie kutoka kwako msaidizi.) (Nisaa 75)
Enyi maulamaa wa ulimwengu wa Kiislamu; wahadhiri waheshimiwa wa hawza na vyuo vikuu katika nchi za Kiislamu, sasa hivi wafikirieni watu wanyonge wa Ghaza, mkisubiri saa moja baadaye itakuwa ni kuchelewa
Leo hii ulimwengu wa Kiislamu umewekwa katika mtihani mkubwa wa kimungu, watu wasio na ulinzi wa Ghaza wamezuiliwa chakula, na baadhi ya serikali si tu kwamba zimekaa kimya mbele ya mauaji haya ya kizazi, bali zimejitokeza wazi katika kuunga mkono serikali ya kizayuni kiasi kwamba dunia inashuhudia upande mmoja wa ukafiri dhidi ya upande wote wa Uislamu.
Qur'ani Tukufu imeiuamsha Umma wa Kiislamu mbele ya Mayahudi wa wakati wa mwanzo wa Uislamu, na imewatambua Mayahudi kuwa ni maadui wakubwa kabisa kwa watu waumini:
«لَتَجِدَنَّ أَشَدَّ النَّاسِ عَداوَةً لِلَّذینَ آمَنُوا الْیَهُودَ وَ الَّذینَ أَشْرَکُوا»
Hakika utawakuta walio shadidi kuliko watu wote katika uadui kwa walio amini ni Mayahudi na washirikina. (Maaida 82)
Na Qur’ani imefunua hila na njama zao dhidi ya Uislamu, na imehesabu urafiki nao kuwa ni sawa na kuingia katika safu yao:
«یا أَیُّهَا الَّذینَ آمَنُوا لا تَتَّخِذُوا الْیَهُودَ وَالنَّصاری أَوْلِیاءَ بَعْضُهُمْ أَوْلِیاءُ بَعْضٍ وَمَنْ یَتَوَلَّهُمْ مِنْکُمْ فَإِنَّهُ مِنْهُمْ إِنَّ اللَّهَ لا یَهْدِی الْقَوْمَ الظَّالِمین»
Enyi mlio amini! Msiwafanye Mayahudi na Wakristo kuwa ni marafiki, Wao ni marafiki wao kwa wao. Na miongoni mwenu mwenye kufanya urafiki nao, basi huyo ni katika wao. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wenye kudhulumu. (Maida 51)
Leo hii ukimya wa kila Mwislamu ni khiyana kwa Qur’ani Tukufu na ni kama kuukata mizizi ya Uislamu, leo hii sauti ya Amiri wa Waumini Ali bin Abi Talib (as) inasikika kutoka ndani ya historia:
أَمَا وَ الَّذِی فَلَقَ الْحَبَّةَ وَ بَرَأَ النَّسَمَةَ لَوْ لَا حُضُورُ الْحَاضِرِ وَ قِیَامُ الْحُجَّةِ بِوُجُودِ النَّاصِرِ وَ مَا أَخَذَ اللَّهُ عَلَی الْعُلَمَاءِ أَلَّا یُقَارُّوا عَلَی کِظَّةِ ظَالِمٍ وَ لَا سَغَبِ مَظْلُومٍ…
Ama kwa Yule aliyepasua punje na akaumba nafsi, lau si uwepo wa waliohudhuria na kusimama kwa hoja kwa kuwapo msaidizi, na ahadi ya Mungu kwa maulamaa kuwa wasikubaliane na ulafi wa dhalimu na njaa ya aliyedhulumiwa..
Maneno haya yanaonyesha kuwa cheo na nafasi yoyote katika Uislamu ina thamani iwapo ina faida kwa Umma wa Kiislamu.
Leo hii ni wajibu na jukumu la maulamaa wa umma kuvunja ukimya dhidi ya jinai hii ya wazi na dhidi ya ukimya wa madola ya kisiasa ya nchi za Kiislamu, pamoja na ukimya na kutofanya kazi kwa jumuiya ya kimataifa na taasisi zake, na kupaza sauti kwa ajili ya kuwaokoa watu wanyonge wa Palestina kutoka kwenye makucha ya watawala wavamizi, ili serikali za Kiislamu ziamke kutoka usingizini na zitekeleze wajibu wao.
Leo hii kutojali amri ya Mungu ya kuwasaidia wanyonge ni sawa na kufuru.
Jumuiya ya Walimu wa Hawza ya Qom, pamoja na kulaani dhulma hii kubwa, inawataka maulamaa wa Kiislamu kuwa na kauli moja, mshikamano wa hali ya juu wa Waislamu, na inatangaza kuchukizwa kwao na jinai hizi, huku ikisisitiza umuhimu wa kuvunja ukimya na kujitahidi kuwasaidia watu wanyonge wa Palestina.
«وَ سَیَعْلَمُ الَّذینَ ظَلَمُوا أَیَّ مُنْقَلَبٍ یَنْقَلِبُون.»
(Na wale waliodhulumu watajua ni mgeuko gani watakaogeukia)
Jumuiya ya Walimu wa Hawza ya Qom
Maoni yako