Jumatano 23 Julai 2025 - 17:33
Warsha ya mtandaoni Maalumu kwa ajili kufanya uchunguzi Kuhusu Mageuzi ya Tafiti za Kiislamu katika nichi za Magharibi Kufanyika kwa Lugha ya Kiingereza

Hawza/ Taasisi ya Kimataifa ya Misbah kwa ushirikiano na Taasisi ya Utafiti wa Utamaduni na Fikra ya Kiislamu, inatarajia kuandaa warasha ya mtandaoni (webinar) maalumu kwa anuani isemayo: “Mageuzi ya Tafiti za Kiislamu katika Vyuo Vikuu vya Magharibi ndani ya Miaka 25 Iliyopita.”

Kwa mujibu wa kitengo cha kimataifa cha  Shirika la Habari la Hawza, Taasisi ya Kimataifa ya Misbah kwa kushirikiana na Taasisi ya Utafiti wa Utamaduni na Fikra ya Kiislamu, katika mfululizo wa mikutano yao ya mtandaoni ya kitaalamu, wataandaa kikao cha mtandaoni kikiwa na kichwa cha habari kisemacho: “Mageuzi ya Tafiti za Kiislamu katika Vyuo Vikuu vya Amerika ya Kaskazini na Ulaya katika Miaka 25 Iliyopita.”

Mkutano huu wa kielimu utafanyika kwa lugha ya Kiingereza na utaongozwa na Profesa Liyakat Takim, mhadhiri wa masomo ya Kiislamu katika Chuo Kikuu cha McMaster nchini Kanada, na Hujjatul Islam wal-Muslimin Murtadha Karimi atakuwa msimamizi wa kielimu wa mkutano huu.

Semina hiyi itafanyika Jumatano, 1 Murdad 1404 Hijria Shamsiyya (sawa na 23 Julai 2025), kuanzia saa 11:30 jioni hadi 1:00 usiku kwa saa za Tehran (saa 4:00 hadi 5:30 asubuhi kwa saa za Toronto).

Kiunganishi cha kuhudhuria semina:

https://www.skyroom.online/ch/iict/international

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha