Kwa mujibu wa kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, kundi la maulamaa mashuhuri wa Bahrain, kupitia tamko lililochapishwa kwenye akaunti rasmi ya ofisi ya Ayatollah Sayyid Abdullah al-Ghurayfi katika mtandao wa Instagram, wamelaani kwa maneno makali vizuizi vya kikatili viliowekwa na majeshi ya Kizayuni dhidi ya Ghaza, vizuizi ambavyo vimepelekea njaa kali kwa wakazi wa eneo hilo.
Katika tamko hilo wamesema: “Tunalaani kwa maneno makali mno kuzingirwa Ghaza na kuwaacha njaa watoto, wanawake na wazee wake kitendo ambacho kinafanywa na Wazayuni madhalimu, na tunatoa shutuma kwa hali ya sasa ya Umma wa Kiislamu ambao umeingia katika ukimya na kughafilika kiasi kwamba haujibu kilio cha wanaotaabika wala hauondoi dhulma.”
Maulamaa hao wametilia mkazo kwamba: “Umma wa Kiislamu na Umoja wa kimataifa wana wajibu wa kimaadili na kisheria kuondosha vizuizi hivi dhalimu na kuwafikishia misaada watu wa Ghaza.”
Maoni yako