Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha trjuma cha Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Hassan Musawi, rais wa Jumuiya ya Kisheria ya Mashia wa Jammu na Kashmir, pamoja na maimamu wote wa Ijumaa wa eneo hili, katika tamko lao wametilia mkazo ulazima wa umoja baina ya Mashia na Ahl al-Sunna, na wamewataka watu wa Kashmir kwa kutunza mshikamano na umoja, waandike mustakabali ulio wazi katika jamii ya Kiislamu.
Wanazuoni katika tamko hili wamelitaja suala la umoja wa Umma wa Kiislamu kuwa ndio hitaji muhimu zaidi kwa wakati huu, na wamewataka Waislamu wote wa Kashmir kwa umakini kamili, wavunje njama mbovu za maadui wa Uislamu, na njia pekee ya kukabiliana na njama za kimadhehebu ni kutunza umoja na mshikamano miongoni mwa Waislamu.
Wanazuoni mashuhuri wa Kashmir pia wameashiria mafundisho ya Qur’an Tukufu na Ahlul-Bayt (as), na wameyataja mapenzi, uadilifu na mshikamano kuwa ndiyo misingi ya maisha ya Waislamu. Wametilia mkazo ulazima wa kuepuka kila aina ya tofauti za kimadhehebu, na wakasisitiza kuwa Umma wa Kiislamu unapaswa kwa mshikamano na maelewano kuzikabili njama za maadui na kushikamana na mafundisho safi ya dini.
Katika tamko hili, kuheshimu matukufu ya Ahl al-Sunna, wakiwemo wake watukufu wa Mtume wa Uislamu (saw) na masahaba wa heshima, kumepewa mkazo maalumu, na kufuata mwongozo wa Ayatollah al-Udhma Sayyid Ali Khamenei na Ayatollah al-Udhma Sayyid Ali Sistani kumeonyeshwa kuwa ni njia ya kuleta umoja. Wanazuoni watukufu wamesema kwamba kila aina ya kauli za uchochezi zinazoweza kuumiza hisia za ndugu wa Ahl al-Sunna, si tu kuwa ni kosa, bali pia kwa mujibu wa fatwa za Marjaa’ Taqleed, ni haramu.
Maoni yako