Jumatano 23 Julai 2025 - 17:34
Hali ya janga la Njaa Ghaza

Hawza/ Ukanda wa Ghaza, chini ya kuzingirwa vikali na utawala wa Kizayuni pamoja na Misri, unakabiliwa na janga kubwa la kibinadamu, ambapo jambo kuu kabisa ni njaa ya kiwango cha juu na uhaba mkubwa wa mahitaji ya chakula.

 Shirika la Habari la Hawza - Katika siku za hivi karibuni, picha za kusikitisha zimechapishwa zikionyesha hali ya Ghaza, zikiwa ni ushahidi wa janga la kibinadamu linalojumuisha baa la njaa, ukosefu wa chakula, na utapiamlo unaotisha katika eneo hilo.

Kwa mujibu wa ripoti za mashirika ya Umoja wa Mataifa na taasisi za misaada ya kibinadamu, Ukanda wa Ghaza wenye idadi ya watu wapatao milioni mbili, unahitaji takriban malori 600 ya chakula kila siku, lakini kwa hakika malori yanayoingia ni kati ya 50 hadi 100 tu, nayo huingia kwa kusuasua na kwa kiwango kidogo sana, kuzingirwa huko kumeambatana na vizuizi vya usafirishaji wa bidhaa kupitia mipaka ya ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu pamoja na mipaka ya Misri, jambo ambalo limepelekea familia nyingi kukosa chakula kwa siku kadhaa mfululizo na kuingia katika hatari ya baa la njaa.

Uhaba mkubwa wa chakula, mafuta na maji umeifanya hali kuwa ya mashaka makubwa kiasi kwamba ripoti zinazungumzia njaa kali kwa watoto na watu wazima, hadi vifo vinavyotokana na hali hiyo.
Mashirika ya "UNICEF" na "UNRWA" pia yameonya kwamba kiwango cha utapiamlo kimeongezeka kwa namna isiyowahi kushuhudiwa, huku hospitali zikijaa wagonjwa wenye njaa, na kukosekana kwa dawa pamoja na vitanda vya kutosha, aidha, kutokana na uhaba wa bidhaa na uwezo mdogo wa kifedha kwa wananchi, soko la magendo limeibuka, hali inayowafanya wengi miongoni mwa wahitaji kushindwa kabisa kununua chakula.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha