Kwa mujibu wa Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, Mkusanyiko wa Wanazuoni Wakislamu wa Lebanon walio hudhuria hafla ya kumbukumbu ya Sheikh Rasul Shahud ambaye aliuawa katika shambulio la kigaidi katika maeneo ya viunga vya Homs, hafla hiyo ilifanyika katika kituo cha al-Mujtaba kilichopo Dahiyah ya Kusini.
Sheikh Hassan Abdullah, Raisi wa bodi ya usimamizi ya Jumuiya ya Wanazuoni Waislamu wa Lebanon, alitoa hotuba yake katika hafla hiyo na kusema kuwa: “Leo tumekusanyika kwa ajili ya kumkumbuka mwanazuoni mkubwa kutoka Syria, mtu ambaye hakuhusika katika mauaji wala kutoa fatwa za kuua, hakuhusika katika dhulma, wala kuchochea uhasama dhidi ya makundi mengine au matabaka ya Kiislamu. Bali alikuwa ni mlinganizi wa umoja wa Kiislamu na aliuchukulia umoja huo kuwa msingi mkubwa katika kujenga Umma wa Kiislamu na mshikamano wa kitaifa. Kwa kuzingatia kuwa watu wa Syria wanajumuisha madhehebu na makundi mbalimbali ya kidini, na kwamba Syria haiwezi kujengwa ila kwa umoja wa watu wake, basi sisi tunatekeleza jukumu hilo.”
Akaongeza kwa kusema: “Kile kinachoendelea leo nchini Syria – kuanzia mauaji ya kishujaa dhidi ya Sheikh Rasul Shahud hadi mashambulizi dhidi ya walio wachache wanaojiita makundi ya ndani – si chochote ila ni njama za maadui wa taifa hili kwa ajili ya kueneza mgawanyiko na mfarakano, na kuchochea mizozo baina yao, ili adui wa Kizayuni aweze kukamilisha udhibiti wake juu ya eneo zima.”
Maoni yako