Jumapili 13 Julai 2025 - 23:05
Hizbullah ya Lebanon yalaani mauaji ya Sheikh Rasoul Shahhoud katika viunga vya Homs

Hawza/ Hizbullah ya Lebanon, katika tamko lake, imelaani jinai ya kikatili ya kulengwa mwanazuoni mashuhuri Sheikh Rasoul Shahhoud katika viunga vya Homs.

Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjuma cha Shirika la Habari la Hawza, Hizbullah ya Lebanon, katika tamko lake, imelaani jinai ya kikatili ya kulengwa mwanazuoni mashuhuri Sheikh Rasoul Shahhoud katika viunga vya mji wa Homs, jinai iliyotekelezwa kwa mikono ya wahalifu na wasaliti wanaotafuta kuyumbisha umoja na umadhubuti wa Syria, na kuwasha moto wa fitna za kimadhehebu na kikabila miongoni mwa wananchi wa taifa hilo.

Hizbullah imesema:

Jinai hii kubwa ambayo imelenga shakhsia ya kielimu na kidini, aliyejitolea muhanga maisha yake yote katika kuitumikia dini na jamii, akiwa ni mlinzi wa madrasa ya Qur’ani, mlezi wa vijana katika njia ya kielimu na kiimani, mlinganiaji mwaminifu wa haki, na mtetezi wa wanyonge, inahitajika kulaaniwa kwa wingi na taasisi mbalimbali za kielimu, vyuo vikuu na taasisi za kiroho.

Hizbullah katika hitimisho lake imesisitiza kuwa: Tunasisitiza juu ya ulazima wa kuwafuatilia na kuwahukumu wahalifu hawa, pamoja na kila aliyethibitika kuhusika au kushirikiana katika jinai hii ya kutisha. Tuna uhakika kamili kwamba watu wa Syria watakataa fikra hii ya kigaidi ambayo inatishia umoja wa jamii, inatibua uthabiti, na inaondoa maoni ya wastani na fikra zenye mwangaza.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha