Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, kuenea kwa mitazamo ya chuki dhidi ya Uislamu na ubaguzi wa rangi nchini Marekani, kulianza kushika kasi zaidi kutokana na kaulimbiu ya kampeni za Trump kuhusu kupiga marufuku kuingia na kuhama kwa Waislamu nchini humo. Takwimu za sasa zinaonesha kuwa hali ya chuki dhidi ya Uislamu imeongezeka kutokana na aina hii ya propaganda za kupotosha.
Mamdani mwenye umri wa miaka 33, atakuwa Meya wa kwanza Mwislamu katika jiji la New York, katika mahojiano ya hivi karibuni na moja ya televisheni mashuhuri ya Marekani, alizungumzia kwa uwazi vitisho alivyopokea wakati wa uchaguzi kutoka kwa watu mbalimbali na wabaguzi wa Kiislamu, na alieleza kuwa kupata nafasi ya kuwa meya ni fursa ya kuwaelimisha watu wote kwamba kuwa Mwislamu ni sawa na kuwa mfuasi wa dini nyingine yoyote ya mbinguni.
Zahran Mamdani, ambaye ni msoshalisti, aliweza kumshinda meya mkongwe na mwenye uzoefu wa jiji la New York kupitia uundaji wa muungano wa vijana waliobobea na wenye ufanisi.
Waislamu wa Marekani katika miaka ya hivi karibuni wamekuwa wakiunda miungano mbalimbali, na hivi sasa inakadiriwa kuwa Waislamu kati ya milioni 3 hadi 4 wanaishi nchini Marekani wakiwa raia halali.
Mamdani amekuwa mmoja wa wakosoaji wakubwa wa uvamizi wa Israel dhidi ya Palestina, na vilevile ni mmoja wa wafuasi wa haki sawa kwa Wapalestina na Wayahudi.
Katika hotuba zake, Mamdani pia amelaani chuki dhidi ya Wayahudi, na ameapa kuwa atakuwa meya mwema kwa Watu wote wa New York.
Maoni yako