Jumanne 1 Julai 2025 - 00:14
Mapambano ya Ayatollah al-Udhma Khamenei dhidi ya ukafiri ni ulinzi kwa Waislamu wote duniani

Hawza / Jumuiya ya Ahladar nchini Uturuki imetangaza kuwa: Mapambano haya ambayo Kiongozi wetu mpendwa, Ayatollah Khamenei, ameanzisha kwa kaulimbiu “Mhimizo wa muqawama unapendelea kufa kishujaa kuliko kuishi kwa udhalili,” ni ulinzi wa heshima sio wa nchi moja tu, bali wa Waislamu wote.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, kufuatia muqawama wa wananchi wa Iran dhidi ya utawala wa Kizayuni na uungaji mkono wa Marekani kwa jinai za Wazayuni, Jumuiya ya Ahladar ya Uturuki imetoa taarifa rasmi.

Bismillahir Rahmanir Rahim

“Basi mpigeni kama anavyowapiga.” (Al-Baqara / 194)

Muqawama, uwezo wa kuzuia adui, subira, na azma ya kimkakati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mbele ya utawala dhalimu wa Kizayuni na mfadhili wake wa kimataifa – Marekani – imeandikwa katika historia kama ushindi wa kijeshi, kimaadili, kisiasa na wa kimungu.

Katika kukabiliana na mashambulizi yaliyotokea kuanzia tarehe 13 Juni 2025, ambapo madhalimu walikusanya nguvu zao zote kwa siku 12 mfululizo, watu huru duniani na Waislamu wote walitazama kwa fahari na heshima jinsi ambavyo umma mmoja, chini ya uongozi wa Sayyid Ali Khamenei – anayeendeleza njia ya Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi Imam Khomeini – ulivyopambana na kuwaangusha maadui kwa nguvu.

Wananchi wa Iran, kwa msimamo wao wa kishujaa, bila woga na wenye kujivunia, walionesha mfano katika uwanja wa vita; Serikali ya Iran, kwa ulinzi uliosimamiwa kwa subira na basira; na Kiongozi wa Umma wa Kiislamu, Ayatollah Sayyid Ali Khamenei, kwa uongozi wake wa busara, ushujaa na wa kuhamasisha, walilinda heshima ya Umma na kwa mara nyingine tena wakatekeleza kwa vitendo aya hii ya Qur'an:

“Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wale wanaopigana Jihadi katika njia Yake wakiwa safu moja kama jengo lililojengwa imara kama chuma.” (As-Saff / 4)

Mapambano haya ambayo Kiongozi wetu mpenzi, Ayatollah Khamenei, ameanzisha kwa kaulimbiu isemayo: “Mhimizo wa muqawama unapendelea kufa kishujaa kuliko kuishi kwa udhalili,” ni ulinzi wa heshima sio wa nchi moja tu, bali wa Waislamu wote.

Sisi kama Jumuiya ya Ahladar, tunawaombea rehema mashujaa waliotoa maisha yao katika mapambano haya matukufu na kuipamba ardhi kwa damu zao. Tunautakia baraka na ushindi muqawama wa wananchi wa Iran, tunavipongeza kwa dhati vikosi vya Jeshi Jasiri la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi, na wanamapambano wa mhimili wa muqawama.

Utawala dhalimu wa Kizayuni na washirika wake wa kimataifa sasa wanapaswa kufahamu kuwa:

“Na wale waliodhulumu watakuja kujua ni mahali gani watarejea.” (Ash-Shu‘ara / 227)

Ushindi wa Iran ni ushindi wa kila eneo lililodhulumiwa, ni ushindi wa kila muumini wa njia ya muqawama, na ni ushindi wa Waislamu wa Muhammadi. Harakati hii ya kimungu itaendelea hadi kudhihiri kwa Imam Mahdi (aj).

Katika muqawama huu mtukufu ambao, kuanzia tarehe 7 Oktoba 2023, ulibadilisha mwelekeo wa historia, mujahidina wa Hamas na Jihad Islami, kwa kufuata aya: “Wala msimuelekee dhalimu,” walilitetea Msikiti wa Al-Aqsa kwa damu zao. Mashahidi wetu, ambao kila mmoja wao alifuata njia ya Imam Hussein (as) huko Karbala, walifuta fedheha iliyokuwa imeganda kwenye paji la uso la Umma na kwa azma ya Umma wakairudisha minbar ya Msikiti wa Al-Aqsa.

Katika uwanja wa Lebanon, Hezbollah, kwa kaulimbiu: “Nafsi hutolewa kwa ajili ya Quds,” walilinda mstari wa heshima na kuthibitisha kuwa ndugu zao wa Gaza hawako peke yao. Wananchi wa Lebanon, hasa shahidi wa Umma Sayyid Hassan Nasrallah, waliwatoa maelfu ya wanaume mashujaa kwa ajili ya Quds.

Uwanja wa Yemen ulitekeleza kwa mafanikio mzingiro wa baharini dhidi ya utawala wa Kizayuni na kuendelea kulipua maeneo ya Palestina yaliyovamiwa. Katika muktadha huo, Yemen iliingia vitani na Marekani na kuwashinda kwa fedheha. Uwanja wa Yemen pia umetoa mashahidi kwa ajili ya Quds na umejitolea kiasi kikubwa.

Kwa mnasaba huu, kwa rehema na shukrani, tunawakumbuka kwa heshima:

Mujahidina wa Kipalestina waliouawa kishahidi katika Tufani ya Al-Aqsa na mashambulizi ya kinyama huko Gaza,
Mashahidi wote wa muqawama waliotoa roho zao kwa ajili ya Quds huko Lebanon, Syria, Iraq na Iran,
Na makamanda wote wa thamani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran waliouawa kishahidi kwa mikono ya utawala wa Kizayuni.

Uwe hai muqawama katika njia ya Quds!

Uwe hai mhimili wa heshima chini ya uongozi wa Ayatollah Khamenei!

Maangamizi kwa Israel, maangamizi kwa ubeberu wa Marekani!

Jumuiya ya Maulamaa wa Ahlul-Bayt (Ahladar)
24 Juni 2025
Istanbul
Habari kutoka Ahladar

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha